• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SERUKAMBA AAGIZA UTEKELEZAJI WA KUKATA BIMA YA AFYA YA KILA MWANANCHI KUTEKELEZWA

Posted on: August 24th, 2022

Mkuu wa Mkoa  wa Singida Peter Serukamba ameagiza kuanza kutekelezwa kwa agizo lake la kuhakikisha kila mwananchi Mkoani hapo anakuwa na bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa kama hatua moja wapo ya kupambana na adui maradhi.

Akiongea wakati wa kikao cha Menejimenti kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Serukamba amewataka wataalamu wa Idara ya Afya kuanza mara moja kutambua Kaya zote ambazo zitahusika kwenye ukataji wa Bima ya Afya.

Aidha RC Serukamba amesema wataalamu hao pamoja na utambuzi wa Kaya waendelee kutoa elimu na  uhamasishaji juu ya Bima hiyo kwa wananchi ambapo ameahidi kuzunguka Kata zote 136 za Mkoa wa Singida ili kuhamasisha wananchi na viongozi mbalimbali lengo likiwa ni kupata Bima hiyo.

Lengo la kikao hicho ni kuandaa mkakati wa namna ya kuhakikisha kila mwananchi mkoani humo anapata Bima ya Afya ili waweze kufaidi uwepo wa vituo vya Afya na Zahanati ambazo zimejengwa maeneo mbalimbali Mkoani hapo.

RC Serukamba amesema ili Mkoa uweze kuinuka ki uchumi unahitaji kuwa na watu wenye Afya Bora ambayo itapatikana kwa kila mtu kuwa na Bima ya Afya.

Amesema Mkoa inakadiriwa kuwa na Kaya laki tatu (300,000) na endapo kila mwananchi atachangia Bima ya Afya ya SH.30,000 kwa mwaka Mkoa utapata zaidi ya Bilioni 9 ambapo bajeti ya dawa kwa  mwaka ni kiasi cha Bilioni 8 hivyo hakutakuwa na upungufu wa dawa vifaa tiba na vitenganishi.

Hata hivyo RC Serukamba amesisitiza miradi mbalimbali ya kilimo isimamiwe vizuri na iweze kutumika kuleta matokeo chanya kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.

Akitolea mfano Skimu ya Itagata iliyoko Halmashauri ya Itigi Wilayani Manyoni ambayo Serikali imetumia fedha  nyingi kiasi cha Milioni 735 na ilitegemewa kuhudumia wakulima 209 ambapo kwa sasa ina hudumia wakulima wachache na wengine waliendelea kuhodhi maeneo bila kuyatumia.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha Menejimenti kwa lengo la kujadili Mpango Mkakati wa kuhakikisha agizo la kila mwananchi anakata bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo Agosti 24, 2022.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.