Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka viongozi mbalimbali walioshiriki mafunzo ya itifaki ya viongozi wa Kitaifa na usimamizi wa maadhimisho ya sherehe na matukio yanayohusu viongozi wa Kitaifa kutumia mafunzo hayo kuboresha utendaji kazi wao.
Maelezo hayo ameyatoa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhasibu Mkoani hapo.
RC Serukamba amesema Mafunzo hayo yatasidia kuondoa ubabaishaji ulikuwa unafanywa katika eneo hilo ambapo watu walikuwa wakikosea matumizi ya alama za Taifa ikiwemo bendera na wimbo wa Taifa.
"Nimejulishwa kuwa mtapata elimu ya matumizi ya Alama za Taifa hivyo ni matumaini yangu kuwa mtapata ufafanuzi sahihi juu ya maswala ya uwekaji wa bendera na matumizi ya Alama za Taifa kama wimbo wa Taifa" Alisema Serukamba.
Hata hivyo Serukamba alisistiza Mafunzo hayo yatolewe kwa watu wengini kuondoa makosa ambayo yalikuwa yanafanyaki huku akiwataka viongozi hao kuwa mabalozi kwa watumishi wao na kuwapelekea elimu waliyopata ili kuongeza uelewa kwa watu wengi.
"Kwa uzoefu wangu kuhusu masuala haya nimegundua kuna ubabaishaji mkubwa kwa watu kukosea hivyo ni matumaini yangu baada ya Mafunzo haya tatizo hilo litaisha”. RC Serukamba
Mkurugenzi wa Maadhimisho na Sherehe za Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Batholomeo Jungu akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba kufungua mafunzo.
Akimalizia hotuba yake RC Serukamba amesema ifikapo kesho mwisho wa Mafunzo hayo viongozi hao watakuwa na weledi ambao utaongeza umakini mkubwa katika utendaji wa kazi.
Awali akifungua Mafunzo hayo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Exervier Saudi amesema Mafunzo hayo ni ya siku mbili na yanalengea kukumbusha na kubadilisha mawazo kuhusu itifaki ya viongozi na misingi ya maadili ya Taifa.
Amesema Mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi zaidi na yatasaidia katika ulinzi na usalama.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alibainisha kwamba mafunzo hayo yamehusisha Wadau 250 wakiwemo Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa mbalimbali hapa nchini.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.