Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka vijana kutumia teknolojia ya mitandao ya simu kutafuta masoko ya bidhaa zao badala ya kutegemea Serikali kufanya kila kitu.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa ufugaji wa nyuki wa kisasa katika kanisa la Anglikana Muhala unaomilikiwa na vijana wa Wilaya ya Manyoni chini ya shirika la Compassion International Tanzania Dkt. Mahenge amesema yapo mataifa ambayo yanauitaji mkubwa wa asali, mbuzi na ng’ombe lakini hawajaweza kupata kwa utoshelevu kwa kuwa biashara imekuwa haifanyiki ki kamilifu.
Dkt. Mahenge amewataka vijana kuhakikisha kwamba wanatumia simu uwepo wa simu na mitandao ya kijamii kwa lengo la kuuza na kununua bidhaa mbalimbali
Amesema Serikali imetumia fedha nyingi kuwekeza miundombinu mbalimbali ikiwemo mkongo wa taifa ili kundi la vijana lipate kufaidika kupata soko na marifa mapya ya ki biashara.
Aidha amewataka vijana kulinda miundombinu pamoja na miradi wanayotafutiwa na mashirika mbalimbali pamoja na Serikali ili kufikia lengo la kumkomboa kijana na wanakwake kwa ujumla.
Dkt. Mahenge amebainisha kwamba Serikali inatekeleza sharia inayozitaka Halmashuri kutenga asilimia kumi (10%) kwa ajili ya vijana na asilimia 40 % kwa ajili ya wanawake na walemavu hivyo kumtaka Mkurungezi wa Halmashauri ya Manyoni kuhakikisha kwamba asilimia hiyo inatumika kuendeleza vijana wilayani hapo.
Naye Afisa vijana wa Mkoa wa Singida Bwana Fredrick Ndahani pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuzindua mradi wa vijana hao na kuwakabizi vitendea kazi mbalimbali vikiwemo Pikipiki na mizinga vyenye thamani ya shilingi milioni 80.4 amezishukuru Taasisi za dini kwa kuwajali na kuwasaidia vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Hata hivyo Bwana Ndahani amewaomba viongozi hao kuendelea kutumia rasilimali walizonazo kuendelea kuwasaidia vijana.
Mwisho amewataka vijana kuendela kuwa waaminifu ili waweze kuaminiwa na kusaidiwa na jamii inayowazunguka.
Aidha mbali ya uzinduzi wa mradi wa vijana hao mkuu wa mkoa ametembelea mradi wa ujenzi wa zahanati ya maweni, shule ya msiningi sayuni na shule ya sekondari ya Mlewa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.