Mameneja wa Wilaya na Mkoa, Wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini "RUWASA" wameagizwa kutafuta hati miliki ya maeneo wanayojenga visima na matenki ya maji kama njia ya kukwepa migogoro na wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 12.08.2022 na Kaimu kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 Emanuel Ndege Chacha wakati wa kukagua Mradi wa maji uliopo kata ya Mungumaji baada ya kuona mwingiliano mkubwa baina ya makazi ya watu na eneo la Mradi.
Chacha ametoa Siku Saba mchakato huo uwe umekamilika na viongozi wa Mwenge wa Uhuru wapate taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa imeonekana maeneo mengi kutokuwa na hati miliki.
,"Serikali inawekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji lakini baada ya siku chache watu wanaibuka kudai visima vimechimbwa maeneo yao hili halikubaliki,, alieleza.
"Wapo watu hata kama wamelipwa fidia au wameamua kuupisha mradi kwa namna yoyote baadae wanarudi tena kudai, sssa naagiza mtafute hati za maeneo hayo' alisema
Aidha amewataka kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanajengewea uzio kwa sababu za kiusalama na ni sehemu ya usafi wa Mazingira.
Sambamba na hilo kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa ameelekeza kupandwa miti katika maeneo ya vyanzo vya maji na kuzunguka matenki ambayo zitasaidia kutunza mazingira.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.