Kuelekea katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (maarufu kama Mei Mosi),Mkoa wa Singida unatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo nchini Tanzania yatakayofanyika Tarehe Mosi mwezi Mei 2025.
Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 11, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego wakati akizungumza na wadau wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo kimkoa na Kitaifa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mhe.Dendego amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika katika uwanja wa Liti uliopo Manispaa ya Singida, ambayo itatanguliwa na Shughuli mbalimbali ikiwemo v michezo mbalimbali,huku jumla ya watu elfu mbili na miatano (2,500)wakitarajiwa kushiriki kwenye michezo hiyo itakayohusisha watumishi kutoka katika wizara tofauti,taasisi binafsi na za umma,
Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa katika kuendelea kusherehesha shughuli hiyo kutafanyika pia utalii wa ndani ya Mkoa wa Singida,lengo likiwa kuwaonyesha wageni waliofika Mkoani Singida mambo mbalimbali yanayopatikana katika Mkoa huu,ikiwemo fursa zilizopo za kiuchumi na uwekezaji.
Maadhimisho hayo yatapambwa na mambo mbalimbali kabla ya kilele ambapo kutakuwa na Usiku wa Kuku ( kuku festival) Mashindano ya magari, Mashindano na ngumi, maonyesho mbalimbali ya shughuli ambazo wanaSingida wanazifanya, Burudani mbalimbali ikiwemo Ngoma za asili na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakubwa hapa nchini.
Kwa upande wake rais wa Shirikisho la Wafanyakazi,( TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema kuwa kupitia mikakati mbalimbali iliyowekwa kwa kushirikiana na Uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wanategemea sherehe hiyo itafanyika vizuri na itakuwa ni ya kipekee sana kutokana na maandalizi makubwa yaliyoandaliwa.
"Singida ipo tayari kuwapokea wageni wote,wataishi vizuri..wenye hofu na malazi watalala vizuri,kwani maandalizi yamewekwa vizuri sana hivyo karibuni sana Singida kusherehekea Mei Mosi itakayofanya sana"amesema Bw.Nyamhokya.
Siku wa Wafanyakazi duniani maarufu kama Mei Mosi hufanyika kila mwaka lengo likiwa ni kuangalia na kufanya tathimini juu ya haki na usawa kwa wafanyakazi, kuzifahamu na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi pamoja na usalama wao mahala pakazi.
https://youtu.be/3fuA8Uth0vs?si=hKn_fxe1ESWoh2Cd
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.