Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ameongoza kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa Stakabadhi ghalani katika msimu wa mwaka 2023/2024 pamoja na maandalizi ya msimu wa 2024/2025 kwa lengo la kutathmini matokeo, changamoto na faida za mfumo huo wa uuzaji wa mazao.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji,Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Bw.Starnslaus Choaji amesema kuwa jumla ya maghala saba (7)yalitumika kwa kazi hiyo katika wilaya ya Itigi na Manyoni,Ikungi,Singida Manispaa,Singida,Mkalama na Wilaya ya Iramba huku kwa mwaka wa 2024/25 wakitarajia kuwa na maghala mengi zaidi.
Pia aliwasilisha baadhi ya changamoto zinazowakabili katika kuhakikisha stakabadhi ghalani inakwenda vizuri ikiwemo uwepo wa watu kati inayopelekea utoroshwaji wa zao la dengu,usimamizi usioridhisha, migogoro baina ya waendesha maghala,baadhi ya watendaji wa vyama vikuu kutokua na sifa stahiki katika nafasi zao(meneja na uhasibu)na ufinyu wa maghala hasa katika Halmashauri ya Itigi.
Mkuu wa Mkoa Mhe.Dendego akizungumza baada ya kusikiliza changamoto hizo,amewaagiza wasimamizi wa stakabadhi ghalani kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa umoja kwa kuwa na kauli moja thabiti katika kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mfumo wa stakabadhi ghalani,Pia aliagiza COPRA kuwafahamisha wadau juu ya mabadiliko ya Tozo kwa kuuondoa mwongozo walioutoa bila kushirikisha wadau.
Pia,njia nyingine za kukabiliana na changamoto zilizoainishwa ni CEAMCU kuajiri Meneja mwenye sifa,huku SIFACU wakijipanga kufuata taratibu baada ya kupata watendaji wenye sifa stahiki na wenye uzoefu wa msimu uliopita.Kadhalika,Doria zitafanyika katika mageti ya ukaguzi kukagua mazao ambayo hayakupata katika Stakabadhi ghalani.
Katika msimu wa 2024/25 Mkoa utaendelea na utekelezaji wa mfumo huu kwa mazao yaliyopo katika mwongozo ambayoni Dengu,choroko,mbaazi,ufuta na korosho huku kukitarajiwa kuwa na maghala mengi zaidi ambayo yatakidhi mahitaji ya wananchi wote wanaotegemea kunufaika na mfumo huo wa stakabadhi ghalani.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.