Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victoria Ludovick amefanya kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa bima ya afya iliyoboreshwa pamoja na maafisa TEHAMA wa Hamashauri zote za Mkoa ili kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili jitihada za kuongeza wanachama na mapato katika Mkoa huo.
Baadhi ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na utunzaji hafifu wa vitenda kazi katika Halmashauri mbalimbali mkoani hapa ambapo kunaweza kusababisha kutofikia idadi ya wanachama ambao wametegemea kuwasaliji.
Akiongea wakati wa kikaokazi kilichofanyika tarehe 18. 08.2021 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Victoria Ludovick amesema kuongezeka kwa wanachama wa iCHF kunategemea uwezo mzuri wa maafisa waandikishaji na vifaa walivyopewa ili kutumia mifumo ya kielektroniki kikamilifu.
Aidha amebainisha kwamba umuhimu wa vifaa na utunzaji wake ni muhimu katika kuongeza wanachama kwakuwa vina uhusiano na mifumo ya kielektroni.
Amesema Dkt. Victoria ili kuongeza wanchama ni lazima kila mwandikishaji kuhakikisha anatunza vifaa vya usajili alivyokabidhiwa ili viweze kufanya kazi kwa watu wengi zaidi na kufikiwa malengo yaliotarajiwa.
Kwa upande wa Mratibu wa mradi CHF iliyoboreshwa kutoka katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida Bw. Paul John Sangalali amesema mbinu mbadala zinatakiwa kutumika katika kuwashawisha vikundi mbalimbali kujiunga na Bima ya afya iliyoboreshwa.
Amebainisha kwamba bima ni biashara hivyo maafisa usajili ni jukumu lao kutafuta wanachama katika maeneo mbalimbali yakiwemo vikundi vya bodaboda, viwandani, Vyama vya Ushirika, mama lishe na makampuni mbalimbali, vibarua wa ujenzi wa barabara na hata wafanyakazi wa makampuni ya usafi.
Hata hivyo mratibu huyo amebainisha kwamba wataalamu wa usajili wahakikishe wanahusisha kaya ambazo ziliandikishwa na kumaliza muda wake kama njia jingine ya kulinda afya zetu lakini kuongeza mapato ya vituo vya afya.
Aidha Bwana Paul anabainisha kwamba umefika wakati kila mtanzania kuwa na bima ili kumsaidia katika matibabu na kuondokana na mila na desturi za kwamba uwepo wa bima ni kukaribisha magonjwa.
Kwa upande wake Bi Sigilinda Modest Mdemu Afisa uchaguzi Manispaa Singida ametumia uzoefu wake katika bima hizo na kushauri matumizi ya njia za mabango, vyombo vya habari na viongozi wenye ushawishi kuwaelezea wananchi juu ya umuhumi wa bima hiyo ya afya.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.