• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

VIONGOZI WA DINI SINGIDA WATOA MAAZIMIO MAZITO SABA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Posted on: October 22nd, 2020

John Mapepele na Rose Nyangasa, Singida

Kamati ya Amani na Dini mbalimbali Mkoa wa Singida inayojumuisha viongozi wa madhehebu na dini zote imetoa tamko lenye maazimio saba kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu huku ikiwaomba waumini wao kumtanguliza Mungu na Serikali kusimamia amani na utulivu ili kuwapata viongozi bora watakaoingoza nchi katika miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Shehe, Hamis Muhamed Kisuke amesema miongoni mwa maazimio hayo ni kuwaomba waumini wao kutenga siku tatu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili ya juma hili kwa ajili ya kufunga na kuomba ili kuombea uchaguzi upite kwa amani na usalama.

  Mwenyekiti wa Kamati ya  Amani ya  Viongozi wa Dini  na Madhehebu mbalimbali Mkoa wa Singida,(aliyesimama)Hamis Muhamed Kisuke akiongoza kikao ambapo walizungumzia  hali ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu na kuja na maazimo saba. (Picha na Rose Nyangasa).

Maazimio mengine yaliyofikiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na viongozi wa dini katika kipindi hiki kudumisha Amani, kutotumika kwenye majukwaani ya siasa kushabikia viongozi wa vyama vya siasa, kuhubiri Amani,

kuhimiza waumini wao kushiriki kupiga kura na kuhimiza kufuata na kutii sheria za nchi ambapo pia wamesisitiza kuviacha vyombo halali vilivyopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi huo vifanye kazi yake.

Mwakilishi wa dini ya Kiislam (Baraza la Kiislam Tanzania) katika Mkoa wa Singida Shehe, Issa Nassor amesema Amani ikitoweka watakaoumia zaidi ni watoto, wanawake, wajawazito, wazee na watu wenye mahitaji maalum kwa kuwa hawana uwezo wa kukimbia na kujitetea.

Aidha, wamewataka wazazi na walezi wa kila familia kuwaasa vijana kujiepusha na kushawishiwa na watu wanaoitakia mabaya nchi ya Tanzania ambapo ameongeza kwamba baada ya kupiga kura vijana warejee nyumbani kwa kuwa tayari Serikali imeshaweka vyombo maalum kwa ajili kuhesabu na kutangaza matokeo hayo.

“Historia inaonyesha kuwa nchi zote duniani zilizopoteza amani ni nchi ambazo walilewa amani, vilevile tukumbuke kupata amani ni mchakao wakati kuvunja amani ni jambo rahisi kabisa. Nawaomba watanzania wenzangu kutumia vipande vyetu vya kupigia kura kuwachagua Viongozi bora” aliongeza Shehe, Nassor

Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Singida, Sweetbert Njewike (hayupo pichani) wakati akielezea majukumu ya jeshi hilo kwenye siku ya upigaji kura Oktoba 28, mwaka huu. (Picha na Rose Nyangasa).

Mwakilishi kwa upande wa wakristo, Askofu wa Kanisa la TAG mkoani Singida, Gasper Mdimi amesema amani ya nchi ni jambo nyeti ambalo linatakiwa kuchukuliwa kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa lina athari pana kuanzia kwenye ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla na kwamba Bibilia imefafanua kuwa chanzo cha Amani ni Mungu mwenyewe, Haki na Watu wanaomcha Mungu.

Amefafanua kuwa vitabu vyote vitakatifu vinasisitiza kutafuta kuwa na amani na watu wote ambapo na kwamba watanzania wanatakiwa kupendana katika kipindi hiki bila kuangalia vyama vyao vya Siasa na kuiombea nchi yao ipate viongozi ambao watailinda amani.

Pia amesema wakati wananchi wanakwenda katika siku za mwisho wa kuhitimisha zoezi la kuwachagua viongozi ni muhimu kuzingatia kuacha kuongea maneno ambayo yatasababisha machafuko na uvunjifu wa amani.

Mwakilishi wa Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida, Padre Padri Elia Mnyakanka amesema Uongozi Bora ni tunu na zao la amani na kwamba ili kuwa na maendeleo na ustawi kuanzia ngazi ya familia na taifa ni muhimu kwa wananchi kutafakari kwa kina na kuwachagua viongozi wanaoweza kuilinda amani.

Akitoa mfano amesema katika taifa la Israel uongozi bora ulikuwa ni nyenzo ya kuwafikisha kwenye nchi ya ahadi kupitia manabii mbalimbali ambapo kwa kufanya hivyo amani ilipatikana.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwapa elimu ya uraia waumini wao ili kuwapa uwezo wa kuwachagua wagombea makini kupitia ilani zao ambapo amesisitiza kwamba uchaguzi wa haki na amani ndiyo njia pekee ya kujitawala na kuleta amani katika nchi.

Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Singida, Sweetbert Njewike majukumu ya jeshi hilo kwenye siku ya upigaji kura Oktoba 28, mwaka huu. (Picha na Rose Nyangasa).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema kwenye kipindi hiki cha uchaguzi majukumu yao ni pamoja na kutunza na kudumisha Amani, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kubaini makosa ya jinai, kuwakamata wahalifu wanaohatarisha amani na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, kulinda mali za raia, kutoa ulinzi kwa maafisa na vituo, pia kuhakikisha hakuna mtu anaye watishia wapiga kura na kuhakikisha usalama wa vifaa vya kupigia kura.

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Rehema Nchimbi amewashukuru viongozi hao kwa kuandaa mkutano huu ambao umelenga kudumisha amani na kuwahimiza wananchi washiriki kikamilifu kupiga kura ili kuwa chagua viongozi bora.

Aidha Dkt.Nchimbi amewataka Viongozi wa Dini kutotumika kuharibu amani na mshikamano ambao upo kwa kipindi kirefu sasa hapa nchini kutokana na kazi nzuri ya kusimamia amani hiyo iliyofanywa na Serikali.

http://singidars.blogspot.com/2020/10/viongozi-wa-dini-singida-watoa-maazimio.html

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.