• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Waratibu wa Miradi Singida Wafundwa

Posted on: November 20th, 2021

Wasimamizi na waratibu wa miradi mbalimbali ya kijamii Mkoani Singida wametakiwa kuongeza juhudi katika usimamizi kwenye utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa jamii husika kama inavyotegemewa.


Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi. Dorothy Mwaluko alipokuwa anafungua  Kikao kazi cha Mradi wa timiza malengo awamu ya pili kilichofanyika Katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo amesema wanufaika wa miradi hiyo wanatakiwa kuhitimu na kufikia mwisho ili wengine waweze kupata huduma hiyo.


Amesema kuna miradi tokea imeanzishwa imebaki na wanufaika hao hao mpaka inaisha jambo ambalo halipendezi, inapaswa kuwepo  utaratibu wa wanufaika kuhitimu baada ya muda na kupisha  wengine badala ya kuendelea kuwakumbatia  alibainisha Mwaluko.


Akitole mfano Mradi wa TASAF amebainisha kwamba waliopewa mitaji wanatakiwa kufika wakati wajiendeze wenyewe badala ya kusubiri msaada kutoka Serikalini kila wakati ili kuendeleza  miradi yao kutoa fursa kwa wengine kupatiwa mtaji hiyo.


Aidha  Mwaluko amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha miradi  wanajamii wanayoianzisha ni ile waliyopendekeza  wenyewe ili iwe rahisi kuisimamia vizuri  huku akiwataka maafisa hao kuendelea kuwasimamia na kuwashauri katika miradi waliyochagua.


Hata hivyo amezitaka Halmashauri kutumia asilimia kumi za fedha wanazozitenga kwa ajili ya wananwake, vijana na walemavu  kuwakopesha vijana  walioanzisha miradi na kuonekana kupiga hatua.


 RAS huyo akamalizia kwa kutoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia kuwezesha wenye mahitaji  kupitia miradi mbalimbali kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu.


Mratibu wa masuala ya UKIMWI  Mkoani hapo Bw.H.Samiti amesema kwamba Mradi huo ulishamalizika awamu ya kwanza na Sasa wameanza awamu ya pili kwa kuendelea kuwanoa wataalamu mbalimbali ambao watatoa elimu mbalimbali kwa vijana.


Amesema vijana wengi wamenufaika na Mradi huo kwa awamu ya kwanza hivyo wanategemea kuwawezesha vijana wengine kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ili kuwasaidia vijana hao kufikia malengo.


 Eriko Kiwanga ni Mratibu wa Shirika la TACAIDS  anasema Katika Mradi wa  timiza malengo awamu ya kwanza umefanikiwa kwa kiasi kikubwa Katika kuwasaidia vijana walioko ndani na nje ya shule katika kujitambua na kupambana na kuepuka magonjwa ya uzazi na UKIMWI kwa kiasi kikubwa.


Amesema pamoja na mafanikio hayo Mradi umekuwa na changamoto ndogo ya namna ya utoaji wa mitaji ambayo ilikuwa ikitolewa kwa awamu mbili na kusababisha bàadhi ya vijana kushindwa kufanya vizuri kwa kuwa fedha zilikuwa zikija nje ya msimu hasa kwa wale wanaofanya miradi ya Kilimo


Amesema Katika awamu ya pili Shirika limeboresha mambo mengi ikiwepo kutoa elimu kwa Maafisa ugani pamoja na kuleta fedha hizo kwa wakati pamoja na kuongeza usimamizi ili kuleta tija iliyo kusudiwa.


Naye Mariamu Omari Mkazi wa Manispaa ya Singida ni moja ya wanufaika wa Mradi wa Timiza malengo awamu ya kwanza ambaye  pamoja na kushukuru Mradi huo kwa kuweza kubadisha Maisha yake ambapo anajihusisha na saluni ya kike na urembo ameiomba Serikali kuongeza kiwango Cha mitaji kwa kuwa kiasi Cha laki nne kinachotolewa ni kidogo kwa kuanzisha Mradi.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.