Shughuli kuu ya kiuchumi ya wananchi wa Mkoa wa Singida ni kilimo. Karibu 80% ya wakazi wa Mkoa wa Singida hujishughulisha na kazi za kilimo kwa kuzalisha mazao ya chakula ambayo ni mtama, uwele, jamii ya mikunde na mpunga.
Mazao ya biashara yanayolimwa ni alizeti, pamba, ufuta na vitunguu na viazi vitamu ambapo zao kuu la biashara ni alizeti. Shughuli nyingine ya kiuchumi inayotegemewa na wakazi wengi ni ufugaji wa mifugo ambayo ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku wa asili na nyuki.
Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia 2014/2015 hadi 2016/2017 ni; mwaka 2014/2015 tani 298,209.055, mwaka 2015/2016 ni tani 762,201.90 na kufikia Juni mwaka 2016/2017 ni tani 457,104.7 Uzalishaji umekuwa ukibadilika kwa kushuka na kupanda kutokana na mvua zinazonyesha kuwa kidogo na mtawanyiko wake kuwa sio wa kuridhisha.
Uzalishaji wa mazao ya biashara mpaka kufikia Juni mwaka 2016/2017 ni tani 1,288,532. Kulingana na makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2017, Mkoa wa Singida unakadiriwa kuwa na idadi ya watu 1,551,766.
Mahitaji ya chakula kwa mwaka kwa wakazi wa Mkoa wa Singida (watu 1,551,766) ni tani 424,795.9. Takwimu hizi za uzalishaji ni hadi kufikia Juni 2017, maeneo mengine bado uvunaji unaendelea.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.