Uchimbaji wa Madini
Mkoa umejaliwa kuwa na madini katika meneo mbalimbali yapatayo 46. Madini yanayopatikana ni dhahabu, shaba, chuma, Titunium; urani, zircon, quartz, amethyst, garnment, kimbertic, almasi, madini ya chumvi, kifusi, mawe, gypsum, kokoto na mchanga.
Kwa kiasi kikubwa uchimbaji unafanywa na wachimbaji wadogo. Usimamizi wa Sekta hii hufanywa na Ofisi za Kanda za Madini. Kwa sasa ipo Kampuni inayoitwa Shanta Mine ipo kwenye mchakato wa kufungua mgodi wa kati wa kuchimba madini ya dhahabu eneo la Sambaru katika Halmashauri ya Ikungi.
Uzalishaji na thamani ya madini kwa mwaka 2016/2017
Madini ya ujenzi uzalishaji wake ulikuwa tani 34,102.50 zenye thamani ya Shs 125,500,000, madini ya jasi uzalishaji wake ulikuwa tani 5,290.83 sawa na Shs 411,341,666.67, na dhahabu uzalishaji wake ulikuwa ni gram 31,383.26 sawa na Shs 2,089,659,445.5 na hivyo kufanya jumla ya mapato ya Shs 2,626,501,112.17.
Jumla ya mrabaha uliotolewa kwa mwaka 2016/2017 ni Shs 115,052,531, kwa madini ya dhahabu ni Shs 83,592,531.29, madini ya jasi ni Shs 12,437,000 na madini ya ujenzi ni Shs 19,023,000.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.