Ufugaji ni shughuli kuu ya pili ya kiuchumi Mkoani Singida. Inakadiriwa kwamba asilimia 11 ya pato la Mkoa linatokana na shughuli za ufugaji.
Mkoa una rasilimali kubwa ya mifugo ambapo kuna jumla ya ng’ombe1,037794, mbuzi 663,560, kondoo 308,578, nguruwe 17,054, punda 38,825, kuku 2,056,714, Bata 18,564, Sungura 3,510, kanga 23,316, Mbwa 50,787 na Paka 24,000.
Mifugo hii licha ya kuwapatia kipato lakini pia inachangia lishe, usafirishaji, kutumika kama benki ya dharura, na Ng’ombe wamekuwa wakitumika kama wanyama kazi katika kukuza kilimo.
Aidha, kutokana na wingi wa Mifugo kumekuwepo na uzalishaji wa Nyama, Ngozi na Maziwa hivyo kuna fursa ya kuwekeza katika Viwanda vya nyama na ngozi. Ufugaji wa kuku kwa asilimia kubwa umeenea Mkoani kote na karibu kila kaya ina Kuku.
Miundombinu ya mifugo iliyopo
Ili kumwezesha mfugaji kuwa na soko la uhakika wa mifugo, Halmashauri zimekuwa zinaendesha minada ya mifugo 46 ya ukwanza (primary markets) na mnada 1 wa upili (secondary market).
Minada hii inaendeshwa kila mwezi. Aidha, kuna majosho 144 ambayo mengi hayafanyi kazi kutokana na kuwa mabovu, malambo 68, machinjio makubwa 3, machinjio ndogo 72, vituo vya mifugo (veterinary centres) 3 na maduka ya dawa za mifugo 12.
Malisho na Ardhi
Eneo la malisho linalofaa kwa ajili ya mifugo linakadiriwa kuwa na Hekta 1,974,700. Eneo hili kitaalamu linatosheleza kufugia mifugo (Lu) 493,675, ukilinganisha na idadi ya mifugo iliyopo sasa.
Hata hivyo hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kukabiliana na tatizo hili. Hii ni pamoja na kuwaelimisha wafugaji wabadili mfumo wa ufugaji huria na kufuga ufugaji wa tija na kibiashara. Serikali za Vijiji/Kata kuwa na mpango wa matumizi bora ya Ardhi, ambapo hadi sasa takribani hekta 30,350 za malisho zimetengwa kupitia mpango huu.
Kuboresha maeneo ya malisho yaliyotengwa na kuwashawishi wafugaji kuongeza muda wa kulisha mifugo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.