Ufugaji nyuki katika Mkoa umesaidia kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja hasa wale waliopo karibu na maeneo ya misitu ya asili.
Ufugaji nyuki katika Mkoa hufanyika kwa njia za asili kwa asilimia 98 na asilimia 2 za njia ya kisasa. Mpaka kufikia mwaka 2017 Mkoa ulikuwa na mizinga ya asili 127,430 na ya kisasa 12,321. Mizinga hii inamilikiwa na watu binafsi pamoja na vikundi vipatavyo 145.
Kati ya vikundi hivi, 11 tu ndivyo vimesajiliwa kama Vyama vya Ushirika. Vikundi vingine bado havijasajiliwa na Mkoa unaendelea na juhudi za kuwahamasisha waweze kujisajili.
Shughuli za ufugaji nyuki hufanywa kwenye maeneo ya wazi na misitu ya asili ya hifadhi ya ardhi za Kijiji yenye ukubwa wa hekta 530,325 vikiwemo vichaka vya Itigi (Itigi thickets).
Aidha, Mkoa wa Singida unaendelea kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti ambalo pia ni chanzo kizuri cha uzalishaji wa asali.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.