Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego ameongoza kikao cha tathmini ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka 2024/2025 pamoja na kujadili bajeti pendekezwa kwa mwaka mpya wa 2025/26
Lengo lakikao hicho ni kuwasilisha, kupitia na kujadili tathmini ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka 2024/25 katika Halmashauri ikiwemo mapato yaliyoidhinishwa, makusanyo halisi na ufanisi,uchangiaji wa mapato ya ndani katika mifuko ya asilimia kumi ikiwemo upelekaji fedha za mikopo ya asilimia kumi kwa makundi husika.
Pia wajumbe wamejadili kuhusu miradi ya mapato ya ndani, changamoto na mikakati ya kuboresha utekelezaji wa bajeti pamoja na kujadili mapendekezo ya makisio ya mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026.
Akizungumza na wajumbe wa menejimenti ya Mkoa,Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi baada ya wasilisho la bajeti,Mhe.Dendego amesisitiza utendaji bora wa kazi kwa watumishi kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha kazi inaendelea mbele kwa kuzingatia utu na ushirikiano huku akiagiza viongozi kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati.
Pia ametoa maelekezo ya uandaaji mzuri wa bajeti mpya kwa kipindi kijacho kwa kuhakikisha zinagusa maeneo muhimu yatakayoleta maslahi mapana kwa jamii wanayoiongoza ikiwemo kutumia vizuri fedha za miradi kwa kuhakikisha miradi mipya na kiporo inafanyiwa kazi na kukamilika kwa wakati muafaka na jamii kunufaika nayo mfano miradi ya ujenzi wa vituo vya Afya na shule.
Kikao hicho kilichofanyika Mkoani Dodoma kimehudhuriwa na Viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Wakuu wa wilaya , makatibu Tawala wa wilaya Wakurugenzi,Wakuu wa Idara na Vitengo, wahasibu , mipango na uratibu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.