Baraza la madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi limeridhia kuipokea kampuni ya SOLDECOM AGRO L.T.D kampuni zawa ya kitanzania inayojihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara ikiwemo biashara ya hewa ya ukaa hapa Tanzania na nchi nyingine pia.
Akizungumza katika baraza hilo tarehe 06 Februari, 2025 Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ally J. Mwanga amesema kuwa Ikungi ilipata nafasi ya mafunzo ya uzalishaji ya hewa ya ukaa kupitia Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika kutokana na uwepo wa misitu katika Wilaya ya Ikungi sawa na Tanganyika na inauwezo wakuzalisha hewa hiyo ili kiwe chanzo cha mapato.
" Tumeridhia kwa moyo wote kupata wawekezaji hawa wa SOLDECOM AGRO LTD ili hewa ya ukaa iweze kuzalishwa katika Wilaya ya Ikungi hususani msitu wa Minyughe na Baadae wakiridhia msitu wa Mlilii" alisema Mhe, Ally Mwanga
Akiwasilisha taarifa katika baraza hilo mratibu wa hewa ya ukaa Bwana Barakael Solomon amesema kuwa Kupitia mradi wa kuhifadhi msitu wa Minyughe tutaweza kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanatokana na ongezeko la joto duniani.
" Tunakwenda kupanda miti palipokatwa miti hasa maeneo ya pembezoni mwa msitu pia kuulinda msitu usivamiwe na kuharibiwa na watu ili uweze kujizalisha upya"amesema Bwana Barakaeli.
Kampuni hii imesajiliwa kisheria kupitia BRELA ,Pia taasisi ya kudhibiti na kuratibu shughuli za biashara ya hewa ya ukaa yenye makao yake makuu mkoani Morogoro yaani National Carbon Monitoring Centre (NCMC) ambayo ndio inayotoa mwongozo wa namna biashara ya hewa ya ukaa inavyofanyika nchini.
Pia,baraza hilo limejadili taarifa za mapato na matumizi na kuhimiza juu ya ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.