• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

*BONANZA LA "MWALIMU NA SAMIA"LAFANYIKA SINGIDA.

Posted on: November 23rd, 2024

Bonanza lililowakutanisha waalimu kutoka Halmashauri mbili za Mkoa wa Singida,Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Singida lenye Jina la "Bonanza la Mwalimu na Samia"lililofanyika katika uwanja WA Bombadia mkoani Singida limefanyika mkoani Singida likiratibiwa na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Singida.


Katika Bonanza hilo Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,ametoa pongezi Kwa waalimu hao kama daraja imara kati yao na wanafunzi katika nyanja za masomo Kwa kuwajengea uwezo imara na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata ufaulu mzuri unaowawezesha kuendelea na masomo ya Sekondari na vyuo vikuu pamoja na msingi imara wa kujiajiri hata baada ya kumaliza masomo yao.

Amesema kuwa serikali inautambua mchango mkubwa WA waalimu na hivyo serikali itakuwa tayari wakati wote kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero zao ili kuendelea kuzitafutia ufumbuzi ili kuendelea kuwaunga mkono Kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi Kwa kujenga miundombinu Bora kuanzia shule ya awali na Sekondari na kuongeza vitendea kazi vya kutosha mashuleni.

"Waalimu wa Mkoa wa Singida mmeendelea kuwa baraka katika Mkoa huu  kwani takwimu za ufaulu katika Mkoa wa Singida zinazidi kupanda juu tofauti na ilivyokua katika siku za nyuma kwani mnafanya kazi zenu Kwa weledi na uzalendo pamoja na changamoto zilizopo ambazo zitafanyiwa kazi"alisema Mhe.Dendego

 Mkuu wa Wilaya ya Singida,Mhe.Godwin Gondwe akizungumza katika Bonanza hilo,amesema tuzo mbalimbali zinazotolewa Kwa waalimu ni kama motisha na zitasaidia kuongeza morali katika ufundishaji na kuwapongeza Kwa matokeo mazuri ikiwemo ya kidato Cha nne mwaka huu yaliyopanda ufaulu Kwa asilimia huku kukiwa na malengo ya kufuta daraja sifuri Kwa mwaka ujao wa 2025.


"Mpango wetu ni  kuondoa daraja ziro kabisa mashuleni,hili litafanyika pia Kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata vyakula mashuleni wote Kwa ujumla na sio Kwa madarasa ya mitihani pekee."alisema DC Gondwe

Naye mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu amesema serikali inaendelea kuunga mkono elimu Kwa kuhakiisha Kuna miundombinu Bora ya elimu kama kujenga mashule,madarasa ya kutosha,nyumba za waalimu,mabweni kufuta ada za wanafunzi kuanzia awali mpaka kidato Cha sita na kuongeza mikopo ya elimu ya juu ili kuwawezesha wanafunzi katika gharama za ada na kujikimu,Hivyo ni vema kuutambua mchango wa mwalimu kwa mkono mwalimu kwani ndie daraja la kuwezesha mafanikio ya wanafunzi.

"Ufaulu katika matokeo umeongezeka Kwa takribani asilimia Tano,hii ni kutokana na uboreshwaji WA mazingira ya kujifunzia na kufundishia Kwa waalimu na wanafunzi,ndio sababu ya mwitikio na hamasa kubwa inayoonekana Kwa waalimu kujitokeza Kwa wingi SIKU ya Leo kwasababu wana furaha kwani changamoto zao zinafanyiwa kazi."amesema Mstahiki Meya.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.