Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema asilimia 10 tu ya watu wazima mkoani Singida ndio wanaotumia huduma za benki kiwango ambacho kipo chini ukilinganisha na kiwango cha kitaifa ambacho ni asilimia 22.
Kaimu Meneja msaidizi sera na chambuzi za huduma za kifedha kutoka BoT, Edmund Mbokosi alisena hayo Leo katika kikao cha kujadili changamoto za kifedha na utatuzi wake Mkoa wa Singida ambacho kimewashirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na mameneja wa benki zinazotoa huduma za kifedha mkoani hapa.
Amesema katika huduma za kifedha Mkoa wa Singida wanatumia asilimia 50 wakati wastani wa kitaifa ni asilimia 72,bima ni asilimia 5,huduma za vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) Singida ni asilimia 7 wakati lengo la kitaifa ni asilimia 12.
Mbokosi amesema kutokana na changamoto hiyo BoT imemua kuja kutoa elimu ili kuangalia namna ya kuweza kupandisha kiwango cha matumizi ya huduma za kifedha katika mkoa wa Singida kwa lengo la kuufanya mkoa kupanda kiuchumi na kuondoka katika nafasi ya tatu kutoka mwisho.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego, amesema mkoa utajitathimini kwenye sensa kwa kupita kwenye maeneo mbalimbali kama kwa wanafunzi mashuleni na vyuo vilivyopo mkoani hapa ili kupandisha kiwango cha huduma za benki.
"Tuna vyuo vingi na taasisi nyingi na karibia kila mtu anatakiwa kulipwa pesa kupitia benki na hivi sasa kuna huduma mpya mfano ya mfumo wa stakabadhi ghalani kwa hiyo nina imani kiwango acha asilimia 72 cha huduma za kifedha tutakifikia," alisema. Ok Google
Awali Mchambuzi Maswala ya fedha kutoka BoT, Michael Mwaituka, alisema BoT imejipanga kuwasaidia wajasiriamali nchini kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (ECGS) pamoja Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SME-CGS).
Amesema lengo la kuwezesha sekta binafsi wenye miradi mizuri kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha zilizosajiliwa chini na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha 2006, pale wanapokuwa na upungufu wa dhamana.
Mwaituka amesema kuwa BoT wanasimamia Mfuko wa Udhamini wa Mkopo kwa niaba ya serikali ili kuwasaidia watanzania kupata mitaji kuongeza uzalishaji, ajira, fedha za kigeni na pato la Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati una lengo la kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati wenye miradi mizuri lakini wana upungufu wa dhamana, kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.