Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dk.Fatuma Mganga, ameishauri mahakama kutumia mahakama tembezi kuwafikia wananchi wa vijijini ambao wanashindwa kufika mijini kupata msaada wa kisheria kutokana na shida mbalimbali zinazowakabili.
Akizungumza juzi wakati wa wiki ya sheria aliwataka viongozi wa mahakama ya Singida kufika vijijini kwani wananchi wengi wa matatizo mengi na wamekuwa wakikosa haki zao za msingi za kuhudumiwa.
"Vijijini hakuna mahakama za mwanzo wala za wilaya kwa hiyo niwashauri na niwaombe zile 'mobile courts' ambazo zimeanzishwa sasa ni wakati wake twendeni kule vijijini na vitongoji kusikiliza matatizo ili kuwapunguzia adha zinazowakabili,"alisema.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Singida,Allu Nzowa, alisema taasisi za haki jinai zina mchango mkubwa katika kulinda amani na utulivu,kukuza utawala wa sheria,kukuza uchumi na biashara ya uwekezaji.
Alisema taasisi hizo pia zina nafasi ya kujadili na kutathimini mambo yanayoathiri utendaji wao na kuandaa mapendekezo yenye tija yatakayoleta ufanisi na kuboresha mfumo wa utoaji haki nchini.
Naye Mkurugenzi wa Shirika linatoa huduma za msaada wa sheria kwa jamii Singida, Teddy Mande, alisema wananchi wengi wanapoteza haki zao kutokana na kutofahamu nini wakifanye ili kutetea haki zao.
Alisema kutokana na hali hiyo ni wakati sasa kwa taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanajihusisha na utoaji msaada wa kisheria kuongeza kasi ili wananchi waweze kupata haki zao.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.