Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameyataka makampuni yaliyochukua fedha kutoka kwa Wakulima kwa lengo la kuwauzia Pembejeo za kilimo na hawakupata kurudisha fedha hizo mara moja.
Dkt. Nchimbi ameyasema hayokatika kikao cha ALAT kilichofanyika Desemba 6, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo ambacho kiliwakutanisha wajumbe kutoka Halmashauri zote za mkoa.
Dkt Nchimbi alisema haiwezekani makampuni yachukue fedha kwa wananchi halafu wasipatiwe Zana hizo, hivyo Viongozi wa halmashauri wahakikishe wanasimamia maslahi ya wananchi.
"Hizo fedha nataka zirudi kwa Wakulima tena bila makato yeyote, mkulima asikatwe hata senti moja."alisema Dkt Nchimbi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, Ally Minja alisema moja ya makampuni yaliyochukua fedha kwa wananchi kwa lengo la kuwapa Zana za kilimo ikiwemo Matrekta ni pamoja na SUMA JKT ambapo kuna baadhi ya wakulima walitoa fedha zao lakini mpaka sasa hawajapatiwa Pembejeo hizo jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa aliwata watumishi wa Serikali kutumika na sio kukaa kwenye viti maofisini kwani mkoa huo sio wa Mabosi bali ni watumishi.
"Huu mkoa sio wa Mabosi, watumishi tumikeni, ondoeni ubosi watumikieni wananchi."alisema Dkt Nchimbi.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akisisitiza jambo, kutoka kushoto Katibu Tawala wa Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi, Mstahiki Meya Mbua Chima na kutoka kulia Mkurugenzi wa Singida DC RAshidi MAndoa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Mkalama Jamse Mkwega wakati wa kikao hicho.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.