Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga ametoa rai kwa madaktari bingwa wa Mama Samia kutoa huduma bora kwa wagonjwa wote wanaofika kupata huduma hiyo kwa kuhakikisha kila mmoja anapata huduma stahiki na ya kuridhisha.
Ameyasema hayo leo Mei 5,2025 wakati akifungua kambi ya madaktari bingwa inayoanza Mei 5 na kutamatika Mei 9 katika hospitali ya mkoa wa Singida (Mandewa).
"Ni wakati wetu sasa kuonyesha uzalendo wetu katika kuwahudumia wenzetu kwani ni jukumu na wajibu wetu kuwahudumia wote wenye mahitaji kwani mazingira ya kufanyia kazi hiyo yapo vizuri ikiwemo vifaa vya kutosha pamoja na watoa huduma wa kutosha,dawa,majengo ya kutolea huduma na mengineyo mengi , hivyo Uwekezaji wetu ulete matokeo mazuri kwa kutumia jitihada zetu ili kuleta matokeo chanya ya huduma hiyo.
Amesisitiza kutumia lugha nzuri pamoja na kutoa huduma nzuri kwa wahitaji wote wanaofika kupata huduma hiyo ili kuacha alama njema hata baada ya zoezi hilo kukamilika pamoja na kuwapa madaktari wageni ushirikiano wa kutosha kutoka kwa madaktari wa Mkoa wa Singida.
"Tunatoa pongezi kwa Mhe Rais kwa kulifanya jambo hilo kuwa rasmi tofauti na huko nyuma kwani amefanya uwekezaji mkubwa sana katika gharama na vifaa muhimu vya kazi inayosaidia kazi kufanyika "
Pia ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Singida kutumia fursa hii ya madaktari bingwa mkoani hapa ili kuweza kutibiwa magonjwa mbalimbali ambayo yangewahitaji kwenda nje ya mkoa.
Naye mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Victorina Ludovick amesema kuwa madaktari bingwa hao walitoa huduma za kibingwa katika hospitali za halmashauri za Mkoa wa Singida ambapo wagonjwa takribani 2500 walipatiwa huduma.
"Tumewapokea madaktari bingwa hapa mkoani kwa sasa ambapo tumepata fursa hii tuluyoipokea kwa moyo mkunjufu nasi tupo tayari kutoa kile tulichonacho pia kujifunza kutoka kwao"alisema Dkt Victorina.
Akizungumza kwa niaba ya wengine waliofika kupata huduma,Marieta Boju ametoa shukrani za dhati kwa Serikali inayoongozwa na Raisi Daktari Samia Suluhu Hasan kwa kuwajali na kuwaletea madaktari bingwa karibu na maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo kumewapunguzia gharama kubwa za kufuata huduma hizo mbali ikiwemo nje ya Mkoa wa Singida au nje ya nchi kabisa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.