• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

"FIKIRIENI KUJIAJIRI BAADA YA KUHITIMU"- DENDEGO

Posted on: November 22nd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewashauri wahitimu wa taasisi ya Uhasibu Tanzania kufikiri zaidi kujiajiri badala ya kutegemea ajira za serikali na  sekta binafsi.

Mhe.Dendego amesema hayo katika mahafali ya 22 ya chuo cha Uhasibu Tanzania tawi la Singida. , na mahafali ya 13 ya Tawi la Singida, yaliyofanyika chuoni hapo kuanzia ngazi ya cheti hadi uzamili.

“ Nawaomba mfikirie zaid kujiajiri kuliko kuajiriwa vipaji mnavyo kama nilivyoona wanafunzi wakibuni mbinu mbalimbali za biashara kwani licha ya ajira kutoa fursa nzuri lakini kujiajiri kunatoa nafasi ya kuwa mbunifu na uhuru wa kufikia malengo yaliyokusudiwa"alisema Mhe.Dendego.

Akiongelea kuhusu wahitimu 1477 waliohitimu katika fani mbalimbali amesema idadi hiyo ni kubwa na faraja kubwa kwa Mkoa wa Singida hivyo wakiitumia katika kutengeneza ajira kutaleta mabadiliko

Kuhusu baadhi ya wanachuo wanao onyesha ubunifu, Mkuu  wa Mkoa amesema serikali ya mkoa itashirikiana nao kwa karibu ili kuhakikisha wanafikia malengo yao huku akiwataka kutumia mitandao ya kijamii kama jukwaa la kutangaza ubunifu, kukutana na wateja, na kueneza mawazo mapya Badala ya kupoteza muda mitandaoni kwa mambo yasiyokuwa na manufaa kwani mitandao hiyo inatoa fursa kubwa ya kujitangaza, kukuza biashara, na kufikia mafanikio makubwa.

Awali,Mhe. Dendego alianza kwa kuzindua program ya  ‘Masters’ ambayo itapatikana katika kampasi ya Singida huku akipongeza juhudi zinazofanywa na Taasisi ya Uhasibu Nchini (TIA), katika kuboresha miundombinu na kusimamia maendeleo ya Tawi lake la Singida, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la utawala litakalokuwa na ghorofa tano na kugharimu zaidi ya Shilingi bilioni 13.5.

Ameeleza kuwa maboresho hayo yanaashiria ukuaji wa chuo hicho na yanaongeza fursa kwa vijana kujifunza maarifa na ujuzi zaidi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.

“Serikali itaendelea kushirikiana na wanafunzi na uongozi wa chuo hiki. Nawaomba sana mkitumie chuo hiki kujipatia maarifa zaidi kwa ajili ya kuitumikia jamii katika kila nyanja,” alisema Dendego.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William Palangyo, alisema kuwa kuanzishwa kwa shahada ya uzamili katika Tawi la Singida ni hatua muhimu itakayochochea ongezeko la wanafunzi wanaotamani kujiunga na chuo hicho.

“Hadi sasa, tayari tumewasajili wanafunzi 66 kwa shahada ya uzamili, ambao wanaendelea kupata maarifa na ujuzi zaidi kwa manufaa yao binafsi na ya taifa kwa ujumla,” alisema Profesa Palangyo.

Naye Mjumbe wa Bodi ya TIA, Renatus Msangira, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi hiyo, aliwahimiza wananchi kutumia fursa ya uwepo wa chuo hicho kwa kuongeza maarifa ambayo yataboresha maisha yao.

Jumla ya wahitimu 1,477 walitunukiwa vyeti vyao katika ngazi mbalimbali za masomo, zikiwemo cheti na stashahada kwenye fani za mahusiano ya umma, uhasibu, uongozi wa rasilimali watu, usimamizi wa biashara, pamoja na ununuzi na ugavi.



Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.