Wakurugenzi wa Halmashauri wameagizwa kuongeza usimamizi wa fedha za mapato kutoka vyanzo mbalimbali na kuhakikisha hakuna mkusanyaji anaye kaa na fedha zaidi ya siku mbili bila kuipeleka benki.
Maagizo hayo ameyatoa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba leo wakati wa kikako cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo ambapo aliwataka Wakurugenzi kueleza kwa nini mpaka sasa bado kuna wadaiwa (defotars) katika Halmashauri zao.
Aidha amewataka wenyeviti wa Halmashauri kwa kushirikiana na wakuu wa Wilaya kuhakikisha wote wanaodaiwa wanalipa fedha hizo na ikibidi hatua zaidi zichukuliwe kwa kuwapeleka Mahakamani au kufuta madeni ambayo uchunguzi utabaini kukosekana kwa ushahidi.
Amesema maendeleo ya wananchi yanategemea namna ambavyo makusanyo yanavyoongezeka kwa kuwa vinategemeana hivyo kwa kuchelewesha malipo hayo ameelekeza kwamba ni kuwachelewesha wananchi maendeleo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.