Mkoa wa Singida umeendelea kupiga hatua kubwa kwa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati na vyuo vya VETA kila wilaya huku miongoni mwake ikiwa Chuo cha Veta kinachojengwa katika wilaya ya Mkalama kinachogharimu zaidi shilingi Bilioni 1 na milioni 300
Waziri Silaa Wakati akitembelea mradi wa chuo hicho amesema zamani mkoa Singida ulikuwa na chuo kimoja ambacho kiliwalazimu wazazi kutembea umbali mrefu kutafuta nafasi ya watoto kusoma kisha mahali pakuishi wakati wa masomo na gharama za kujikimu tofauti na sasa hivi vyuo hivyo vimejengwa katika kila wilaya na gharama zitapungua sana.
Aidha amewataka wazazi kusimamia malezi na maadili ya watoto ili kuzalisha jamii iliyo bora ili vijana wa Mkalama kuja kufaidi matunda ya chuo kinachojengwa katika kijiji cha mwando na kuwanufaisha Wakazi wanaoshi jirani na chuo hiko
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amesema nje na mipango iliopo katika ujenzi huo wao kama mkoa wanatarajia kuanza ujenzi wa majengo mawili ya mabweni kuanzia mwezi januari mwakani ili kuwarahisishia wanafunzi wanaotaka kusoma chuo hiko kutoka maeneo ya Mbali
Dendego amewahamasisha wananchi kushiriki katika kutoa nguvukazi katika baadhi ya kazi ikiwemo kukusanya mawe na kokoto ili inapofika mwezi wa kwanza ujenzi rasmi wa m
"Sisi kama mkoa tutajiongeza kwa maana ya kuweka mabweni hapa wilaya hii ni kubwa, watakuja watoto watembea kwa miguu lakini wanaotoka kata nyingine lazima walale, mapema januari tunaanza ujenzi wa mabweni”
Loti Kambi mwananchi wa Nkalakala amewataka wazazi na wananchi wenzake kulinda maadili ya watoto wao hasa chuo hiko kitakapoanza kutoa mafunzo kwenye kipindi hiki cha mmomonyoko wa Maadili
“Mimi nawaita wazazi nawapa wito ili tuweze kulea maadili yaweze kuwa mazuri ili tuweze kupata watu wazuri kuja kujifunza hapa”
Katika hatua nyingine Akiwa katika ziara hiohio wilayani humohumo Jerry Silaa amezindua zahanati ya Kijiji cha Igonia wilayani Mkalama mkoani Singida iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2013 na baadae serikali kumalizia ujenzi wa zahati hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 80.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, Waziri Silaa amesema zahanati hiyo imejibu kiu ya changamoto ya wananchi waliokuwa wakikumbana nayo kwa kufuata huduma za afya umbali wa zaidi ya kilomita 10
Amesema zahanati hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia kuwahudumia wananchi ili kutokwenda katika maeneo mengine ya mbali kufuata huduma
Zahanati hiyo ilifunguliwa mwezi wa sita mwaka huu (2024) mpaka sasa imehudumia wakazi 880 huku mpango wa kuongeza wahudumu wa afya katika zahanati ukiwekwa ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.