Wafanyabiashara wadogo Manispaa ya Singida wameshauriwa kujiunga katika vikundi vya wajasiriamali na kuvisajili ili waweze kukopesheka katika taasisi mbalimbali za fedha.
Ushauri huo umetolewa leo Januari 28, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili wakati alipokutana na wafanyabiashara wadogo katika soko la wamachinga la Kata ya Majengo katika Manispaa hiyo alipokuwa akikabidhi fedha kiasi cha Tsh. 2,000,000 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo .
Mhandisi Muragili amesema namna pekee ambayo vijana wataweza kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha maisha yao ni kujiunga katika vikundi ili waweze kuaminiwa na kukopesheka.
Aidha DC Muragili amebainisha kwamba mabenki mbalimbali hapa Singida yakiwemo CRDB, NMB NBC na nyinginezo wameonesha utayari wa kuvikopesha vikundi ambavyo vimesajiliwa hivyo kuwataka vijana kujiunga ambapo Maafisa Maendeleo ya Jamii kusaidia utoaji wa miongozo mbalimbali kufanikisha zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (mwenye suti) wakati alipokutana na wafanyabiashara wadogo katika soko la wamachinga la Kata ya Majengo katika Manispaa ya Singida. Wa kwanza kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu.
Amewakumbusha vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 35 kutumia fursa ya mikopo ya vijana asilimia nne(4%) inayotolewa na Halmashauri kwa kuwa ina mashart nafuu na haina riba.
Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa mbele ya wafanyabiashara hao (wamachinga) DC Paskasi amesema kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya usafi kama ambavyo alivyotoa ahadi hiyo alipokutana nao tarehe 06/11 mwaka jana.
Ununuzi wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa ya kufanya usafi kila jumamosi katika maeneo yanayowazunguka ili kuepuka magonjwa ya milipuko alibainisha DC Muragili.
Katika hatua nyingine Mhandisi Paskasi akawakabidhi fedha Tsh. 1,000,000 (Milioni moja ) kupitia kwa mwenyekiti wa Vijana Mtaa wa Majengo Saidi Hassani kama sehemu ya ahadi ya mkuu wa Mkoa juu ya uboreshaji wa eneo lao la uoshaji wa magari.
DC akatumia muda huo kuwaasa vijana wote kutumia fedha hizo kwa malengo mahususi ili ziweze kuleta chachu katika biashara zao, na zisaidie kuibua miradi mipya ya maendeleo.
Sambamba na hilo DC Muragili akakabidhi shilingi milioni mbili(2,000,000) wa diwani wa Unyianga kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Unyianga ikiwa ni muendelezo wa kukamilisha ahadi alizozitoa kwa wanachi.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa kutekeleza ahadi zake katika vikundi vilivyopo Kata ya Majengo na Kituo cha Afya Unyianga.
Meya huyo amewasihi Maafisa Maendeleo ya jamii ngazi ya wilaya kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wafanyabiashara hao ili kusaidia kutambua fursa ambazo zinawazunguka .
Kwa pamoja viongozi hao wakatoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti litakalozindiuliwa ki mkoa jumamosi tarehe 29.01.2022 katika kingo za ziwa Kindai ili kurejesha mazingira ya ukijani mkoani Singida.
Baada ya uzinduzi huo kila mwananchi atatakiwa kupanda miti katika maeneo wanayoishi na maeneo ya mipaka ya mashamba yao kwa nyakati tofauti aliendelea kueleza Dc Muragili.
DC Muragili akikabidhi shilingi milioni mbili (2,000,000) kwa Diwani wa Unyianga kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Unyianga ikiwa ni muendelezo wa kukamilisha ahadi alizozitoa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge kwa wanachi.
Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili
Mtendaji wa Kata ya Majengo akisoma taarifa kwa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Singida kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla ya utekelezaji wa ahadi ya Mkuu wa Mkoa kwa vijana
Baadhi ya watendaji na vijana wa Kata ya Majengo wakati wa hafla ya utekelezaji wa ahadi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge kwa vijana hao.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.