Wajumbe wa kamati ya Rufani kutoka Wilaya tano za Mkoa wa Singida wamekula kiapo cha utii na uadilifu ,uaminifu na kutunza siri kwa lengo la kuhakikisha haki kwa watu wote kwa mujibu wa sheria,katiba na kanuni katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Tukio hilo limefanyika Novemba Mosi,2024 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Singida likishuhudiwa na Hakimu Fadhili Enock Luvinga.
Akizungumza wakati wa tukio hilo,Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga amesisitiza mshikamano katika kamati za wajumbe wote kwa kufikia makubaliano mazuri yenye tija katika kushuhulikia taratibu zote za uchaguzi kwenda vizuri.
"Mkatumie nafasi zenu vizuri katika kusaidia mkoa wetu ili zoezi zima la uchaguzi liende vizuri na kuridhisha wagombea na wananchi kwa ujumla."alisema
Daktari Mganga amesisitiza wajumbe kupitia kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa lengo la kupata au kuwa na uelewa wa kutosha juu ya kanuni za uchaguzi ili kutoa maamuzi bora yenye tija na kudumisha amani,upendo na mchakato bora wa uchaguzi mkoani Singida,Pia ameahidi kama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo ya rufani wakati wowote utakapohotajika kwa nia ya kuhakikisha shughuli ya uchaguzi inakwenda vizuri.
Nasema Kazeni Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida,akitoa ufafanuzi kuhusu kiapo,amesisitiza kila mmoja akiishi kiapo hicho katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa uadilifu kwani endapo mtu akienda kinyume na kiapo atachukuliwa hatua za kisheria.
"Ikiwa Kiapo ni tamko analotoa mtu ili akubali jambo fulani ,pale Utakapokula kiapo hiki,uadilifu uwe mkubwa sana katikai kazi hii nyeti na kiapo huki kitatumiwa kama kielelezo katika kukuchukulia hatua za kisheria pale utakapokengeuka na kwenda knyume na kiapo hiki"
Sambamba na zoezi hilo,wajumbe wa kamati ya rufani wamekabidhiwa mihuri itakayotumika katika shughuli nzima ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kusisitizwa kuitunza vema ili kuepusha matumizi mabaya kwa watu wasiohusika.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.