Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji akiwa ameambatana na kamati ya usalama wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Miradi.
Ziara hiyo imefanyika leo 11, Disemba 2024 ambapo miradi mbalimbali imekaguliwa ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Shule ya Ufundi ya Sekondari Amali (Kintinku - Lusilile) ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Kamati iyo imekagua ujenzi wa shule mpya ya msingi umoja (Tambukareli), ujenzi wa miundombinu ya kidato cha tano Shule ya Sekondari Manyoni pamoja na Mradi wa Shule mpya ya sekondari Matori (Manyoni).
Dkt.Mashinji ameelekeza kuwa miradi iyo ikamilike ndani ya Wakati ili ifikapo Tarehe 15, Januari 2025 shule zinapofunguliwa wanafunzi waweze kutumia madarasa hayo.
Kamati hiyo imekagua miradi inayotekelezwa katika jimbo la Manyoni Mashariki na ziara hiyo itaendelea kesho ambapo miradi inayotekelezwa katika jimbo la Manyoni Mashariki itakaguliwa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.