Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mhe.Halima Dendego ameshiriki kongamano katika chuo cha Uhasibu kampasi ya Singida lenye jina la Kongamano la wasomi na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Maisha baada ya chuo kwa wasomi wa elimu ya juu na vyuo vya Kati.
Akizungumza katika kongamano hilo,amewaasa wanafunzi hao kutumia vzur ujana wao kwa kesho iliyo bora kwa kuzingatia Uzalendo,heshima,utii,na utulivu na Mtandao wa watu wazuri wenye nidhamu nzuri ili kujiletea heshima katika jamii .
Pia amewasisitiza kujiandaa vizuri kwa kutumia elimu yao wanayopata vyuoni ili kuweza kujiajiri kwani kijana kujiajiri na kujipatia fedha kwa nguvu zake mwenyewe humletea heshima amani na uhuru katika maisha yake.
"Msichague kazi,ni vema kujiajiri ili kuongeza kipato,Tuchakarike vijana kuongeza kipato kwani Ubora na amani ya nchi yetu ni kutupa fursa ya kupata kipato.Ujana ni fedha,nidhamu na kujiamini.Muda wa kuishi vyuo ni mfupi sana hivo tuutumie vzur kuandaa maisha mazuri ya baadae baada ya chuo.
Licha ya hayo amewaasa kuepusha mahitaji makubwa yasiyo ya lazima kwa wanavyuo ili kuepusha gharama zisizo na msingi kwa wazazi wao wanaowagharamia,bali kutumia muda wao mwingi kujisomea kwa bidii na kuepuka mahusiano ya kimapenzi wawapo vyuoni yenye fadhaa mbali mbali ikiwemo kufeli mitihani,vifo kutokana na gomvi za wivu wa kimapenzi na magonjwa ya ngono ikiwemo VVU na UKIMWI.
Awali Amaniel Samweli,akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida,ametoa elimu ya hamasa juu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa akisisitiza kuwa ni haki yao kushiriki kupiga kura na kuwahimiza kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi .
Peter J.Peter rais wa wanafunzi katika chuo cha uhasibu kampasi ya Singida na Godfrey Mtilabu,Katibu Mkuu wa TAHLISO wamezungumza kwa niaba ya wanafunzi wote kuwa wapo tayari kushirikiana na serikali katika zoezi zima la uchaguzi kwa kuhakikisha wanatoa taarifa yeyote yenye viashiria vya kuvunja amani katika sehemu husika kwa lengo la kutimiza wajibu na haki yao ya kidemokrasia.
"Tutaendelea kuwa waadilifu na wazalendo kwa Taifa letu,vijana hatutakengeuka na kupotoka bali tutakua pamoja daima kudumisha umoja na amani ya nchi yetu."amesema Godfrey.
Sambamba na hilo,wanafunzi wamepata elimu ya afya kutoka Shirika la Mega We Care juu ya ugonjwa wa UKIMWI,afya ya uzazi na matumizi sahihi ya dawa,Pia Mkuu wa Mkoa ameahidi kuanzishwa kwa ligi ya vyuo Mkoani Singida.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.