Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amewakaribisha wawekezaji katika mkoa wa Singida kwa kuwahakikishia kuwa Singida ni salama na mahali rafiki kwa uwekezaji wa aina zote.
Ameyazungumza hayo leo Aprili 25,2025 katika mkutano na waandishi wa habari akiwakaribisha wageni na viongozi wote kushiriki sherehe Za Mei mosi Mkoani Singida huku akitaja fursa nyingi za biashara na uwekezaji zinazopatikana mkoani hapa .
Amesema kuwa Mkoa wa Singida una fursa adhimu ikiwemo watu wakarimu,rasilimali watu ya kutosha ikijumuisha idadi kubwa ya wasomi,ardhi nzuri ya mazao kukua vema kama vile alizeti,mpunga,dengu,korosho na mengine mengi.Pia kuna madini ya dhahabu ambayo yanapatikana katika mgodi wa Shanta ambao hivi karibuni utazinduliwa mgodi mwingine ,
Pia Mhe Dendego amesema Singida ni rafiki kwa uwekezaji kwani inafikika kwa urahisi sana kutokana na kuwa katikati ya nchi na miundombinu yake ya bara bara kuwa rafiki.
Ufugaji Mkoani Singda ni fursa kwa sababu ni rahisi kunenepesha mifugo mbalimbali na kusafirisha nyama nje ya mkoa sambamba na Ufugaji wa samaki katika mabwawa ambayo ni rafiki kutokana na uwepo wa maji baridi na salama kwa ufugaji samaki.
"Mkoani Singida tuna Upepo ambao unaweza kuzalisha umeme wa kutosha,pia uwepo wa vichaka adimu duniani vilivyopo Wilaya ya Manyoni ambayo mwekezaji atavuna hewa ya ukaa.Sambamba na hilo nawakaribisha wageni na wawekezaji wote kuchangamkia fursa ya nishati safi za kupikia kwani idadi ya kaya zinazohitaji nishati hiyo Mkoani hapa ni takribani kaya laki nne,hivyo ni fursa kwenu kuja kuwekeza katika kuuza vifaa mbali mbali vinavyohitajika katika majiko ya nishati safi pamoja na ubadilishaji wa mitungi."amesema Mhe.Dendego.
Mkuu wa Mkoa wa Singida ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni wote waliofika mkoani hapa kwa ajili ya mei mosi katika hafla ya utalii wa ndani ambayo watapata nafasi ya kuujua mkoa wa Singida vizuri zaidi,ambayo itafanyika Aprili 27,2025 ambapo watapata fursa ya kutembelea Shemu mbali mbali za kiutamaduni na kupata kuifahamu vema historia ya Mkoa wa Singida,mila na tamaduni na makabila yake
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Singida kushiriki katika siku ya Mei Mosi kwa lengo kubwa la kumpokea na kumpa pongezi za dhati Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na mambo mengi aliyoyafanya katika miradi ya maendeleo na ya kimkakati iliyofanyika Singida ikiwemo sekta ya afya na lishe,elimu, miundombinu na usafirishaji, michezo,maji,biashara na uchumi na mengine mengi ambayo yamekuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla na kurahisisha ubora wa maisha ya wananchi.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amoni Kakwale amewatoa hofu wageni na wananchi wa Mkoa wa kwa kuwahakikishia usalama wao na mali zao kwa muda wote watakaokuwa mkoani Singida kusherehekea Meimosi huku akitoa rai kwa wale wote waliokuaudia kuitumia vibaya Meimosi ili kufanya uhalifu kwani itawapelekea kuchukuliwa hatua kali za kiusalama
Pia ametoa angalizo kwa madereva wote hususan madereva wa magari ya serikali kuhakikisha wanafuata sheria zote za barabarani wakati wanapoendesha vyombo hivyo vya moto ili kuhakikisha usalama wao na wa watu wengine wanaotumia barabara.
Sambamba na maandalizi hayo,Mei Mosi Mkoani Singida linatarajiwa kuwa na usiku wa Kuku ( kuku festival), mashindano ya magari, ngoma za asili, makongamano na bonanza la wafanyakazi ilisindikizwa na kauli mbiu ya Mei mosi 2025
"UCHAGUZI MKUU 2025,UTULETEE VIONGOZI WANAOJALI HAKI NA MASLAHI YA WAFANYAKAZ
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.