Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego amesema kuelekea siku ya Mwanamke duniani kimkoa,wameazimia kufanya matendo ya huruma kwa kutembelea na kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDC .
Mhe.Dendego amesema hayo leo ofisini kwake wakati akizungumzia maandalizi ya siku ya Mwanamke kimkoa ambayo yatafanyika tarehe 7/3/2025 katika uwanja wa Bombadia.
Akitoa ratiba ya matukio mbalimbali yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho,Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kuanzia leo tarehe Mosi,maadhimisho yameanza katika ngazi ya Vijiji, Kitongoji ,Mitaa,Kata, Tarafa na Halmashauri na kuanzia tarehe 5 Machi, maadhimisho yataanza kufanyika katika ngazi ya Mkoa ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika.
Katika Bonanza la Machi 5, kutakuwa na michezo mbalimbali katika uwanja wa Bombadia ikiwemo mpira wa Pete, Ngoma za asili, Muziki wa kizazi kipya, lengo la burudani hizi ni uhakikisha ujumbe wa siku ya Mwanamke kwa mwaka huu unafika kwa umma .
lakini pia tarehe 6/3/2025 kutakuwa na kongamano la wanawake wote kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Mkoa na jumla ya wanawake zaidi ya elfu moja(1000) watakuwepo katika kongamano hilo likisindikizwa na Mada Mbalimbali ambazo zitafundishwa na kujadiliwa kama vile Mwanamke na Uchumi, Nishati safi ya kupikia ,mashaka ya ukatili,Mwanamke na Kodi na uwezeshwaji wa Mwanamke kuwa Mama bora.
Tarehe 7/3/2025 itakuwa ndio kilele cha siku ya Mwanamke kimkoa wa ambapo sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Bombadia zikitanguliwa na maandamano ya Wanawake wote,Burudani mbalimbali na zoezi la utoaji wa tuzo kwa Wanawake waliofanya vizuri katika maswala mbalimbali yanayogusa jamii.
Katika hatua nyingine kueekea mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Mkuu wa Mkoa wa Singida amewaomba wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na Kwaresma ili wawape nafasi ya waumini kupata unafuu wa kupata mahitaji yao katika kipindi hiki.
Siku ya mwanamke duniani inaadhimishwa tarehe 08/03 ya kila Mwaka na kwa Mwaka huu siku hiyo kitaifa itafanyika Mkoani Arusha, kwa Mkoa wa Singida itaadhimishwa tarehe 07.03.2025 katika uwanja wa Bombadia Manispaa ya Singida na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni :
"WANAWAKE NA WASICHANA 2025:TUIMARISHE HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI"
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.