MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amewaangiza Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo kuhakisha kila kata Wakulima wanapata mbolea ya ruzuku aina ya FOMI OTESHA.
Serukamba ametoa maelekezo hayo kwa Wakuu wa Wilaya muda mfupi baada ya kuzindua ghala la kuhifadhi mbolea hiyo ambayo yenye uzito wa Tani Miamoja kwa lengo la kuwafikia wakulima kwa wakati.
Amesema nia ya Serikali kutoa mbolea ya ruzuku kwa Wakulima ni kuhakikisha wanalima kilimo cha kisasa na chenye tija kwa lengo la kutoa faida kubwa kwa mkulima kwa kumuongezea kipato.
Amesema kuwa kwa sasa Singida inatakiwa kuingia kwenye ramani kubwa ya kutambulika kwa kulima mazao mengi ya kimkakati.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa licha ya Singida kuonekana kuwa Mkoa wa Tatu katika kiwango cha umasikini lakini kutokana na juhudi za Serikali kwa kuwekeza katika kilimo ni lazima Mkoa huo uingie katika historia ya kubadilisha hali ya umasikini.
Amesema kuwa kwa Mkoa wa Singida umejipanga kuhakikisha unazalisha mafuta yote ya Alizeti ya kutosheleza mahitaji ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Mbali na hilo amesema kuwa Mkoa wa Singida umekuwa ni Mkoa wa pili kwa mradi mkubwa wa umwagiliaji ambapo kiasi cha shilingi bilioni 34 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.
Kutokana na hali hiyo Serukamba amesema wananchi wa Mkoa wa Singida wanatakiwa kuwa na mwamko kwa kutumia mbolea ya FOMI OTESHA na kuchangamkia kilimo cha umwagiliaji.
Mwisho.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.