Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego ameongoza vikao viwili vya wajumbe wa Kamati za maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi zinazotarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Singida Mei 1,2024.
Vikao hivyo vimefanyika Machi 28 na 29 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa likishirikisha viongozi kutoka TUCTA,akiwemo rais wa TUCTA,Katibu wa TUCTA,Wenyeviti wa Kamati za maandalizi ambao ni wakuu wa Wilaya,na wajumbe mbalimbali.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan huku kukitarajiwa kuwa na mambo mbalimbali ya kuvutia kabla ya tukio kuu ikiwemo michezo ya mashindano ya magari,riadha,Kuku festival,utalii wa ndani na mengine mengi.
KARIBU SINGIDA ,SINGIDA NI SEHEMU SAHIHI KUISHI NA KUTEMBELEA.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.