Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego,ameshiriki katika uzinduzi wa Bodi ya Parole katika ofisi za Magereza Mkoa wa Singida
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Magereza Mkoa imehudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida,Dkt.Fatuma R.Mganga,wajumbe wa Bodi,Kamati ya Ulinzi na usalama mkoa,Pamoja na Sekretarieti.
Akizungumza katika hafla hiyo Mheshimiwa Dendego ameipongeza Bodi ya Parole kwa utendaji mzuri wa kazi huku akisisitiza elimu kutolewa kwa wananchi ili kuelewa kwa undani Zaidi kuhusu majukumu ya Bodi ya Parole na umuhimu wake kwa walengwa wa moja kwa moja ili kuendelea kunufaika na fursa hiyo.
Pia, amesisitiza uhamasishaji kwa wazazi kuhakikisha malezi bora ya msingi kwa Watoto wao katika misingi ya dini,mila,desturi na tamaduni kwani kutofanya hivyo kunaongeza idadi kubwa ya vijana wanaojihusisha na uhalifu na baadhi yao wanaomaliza vifungo vyao hudumu uraiani kwa muda mfupi kwani hujikuta wakijiingiza katika vitendo vya uhalifu na kurejea gerezani.
“wazazi warudi katika majukumunyao ya msingi ya kulea Watoto,tusiache nafasi kubwa kwa Watoto kujifunza katika mifumo kama mitandao ya kujamii,bali tuwalee katika misingi ya dini,mila, desturi na tamaduni zetu”Alisema Mheshimiwa Dendego.
Akizungumza katika tukio hilo,Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Mkoani Singida, Liana A.Hassan ameahidi kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,Menejimenti Katibu wa Bodi na timu yake katika kutekeleza kazi huku akisisitiza utayari katika kufanya kazi na na ushirikiano baina yao kwa maslahi mapana ya Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
“Tutatoa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa kazi hii ambayo tumeaminiwa kuifanya,tuwe na utayari kufanya kazi ambayo Serikali yetu imetuamini kuifanya”Alisema Liana
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Singida,Liana A.Hassan
Katibu wa bodi hiyoambae pia niMkuu wa Magereza Mkoa wa Singida, SACP Khatibu Juma Semzono akizungumza katika uzinduzi huo,amefafanua maana ya Parole kama utaratibu wa sheria unaotoa fursa kwa wafungwa waliofungwa kuanzia miaka minne waliokwisha kutumikia theluthi ya kifungo chao na kuonyesha uelekeo wa kurekebika na tabia nzuri kurudi katika jamii kwa masharti maalumu na kanuni.
Pia,ameambatanisha Vigezo vinavyowawezesha wafungwa kupendekezwa na kunufaika na Parole ambayo ni maoni ya viongozi wa vijiji kama wanakubalika katika jamii au la,aina ya makosa yao waliyoyafanya,maoni ya familia zao,upatikanajiwa waathirika Pamoja na maoni yao hasa kwa jamii ya wafugaji ambaohawana makazi maalum (wanahama hama),upatikanaji wa nyaraka za hukumu na alama za vidole kwa wakati,mienendo na tabia wawapo gerezani na taarifa kutoka kitengo cha upelelezi
Katibu wa Bodi ya Parole na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.