• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

“Miradi yote iliyokuwa inazinduliwa, inafanyiwa ufunguzi, inawekewa jiwe la msingi, inakaguliwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2021 yote imekubaliwa” Dkt. Binilith Mahenge

Posted on: July 25th, 2021

Mwenge wa Uhuru 2021 mkoani Singida 24 Julai, 2021 ulikamilisha mbio zake katika Wilaya ya Manyoni kwa Miradi yote iliyokuwa inazinduliwa, inafanyiwa ufunguzi, inawekewa jiwe la msingi, inakaguliwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2021 yote imekubaliwa.

Julai 25, 2021 Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amekabidhi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati wa kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka, alisema Mkoa wa Singida unamuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii, kutunza amani na utulivu, umoja, mshikamano, mazingira na uhuru wetu hakika kazi iendelee.

Dkt. Binilith Mahenge alisema, Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Singida ulikimbizwa jumla ya Kilometa 642.3, ulipitia jumla ya miradi 55 inayohusu TEHAMA, Elimu, Afya, Mazingira, Maji, Biashara, Barabara na Program za Rushwa, Malaria, Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya, VVU/UKIMWI na Lishe.

Akifafanua zaidi alisema, Miradi 9 ilizinduliwa, miradi 2 ilifanyiwa ufunguzi, miradi 6 iliwekea jiwe la msingi, miradi 36 ilikaguliwa na miradi 2 ilitembelewa. Miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ilikuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 8,182,219,653.99

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa  wakati wa mapokezi ya Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Gery Muro alisema  Mwenge huo utakimbizwa Wilayani hapo kwa muda wa masaa 24 ambapo utakagua miradi mitatu na Programu sita.

Aidha  Mhe. Rahabu Mwagisa  amesema Serikali ina lengo la kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma ya maji vijijini unafikia 85% ifikapo mwaka 2025 kwa hiyo ni jukumu la RUWASA na wadau wengine kushirikiana na Serikali kuhakikisha mpango huo unakamilika.

Hata hivyo Mhe  Rahabu alibainisha kwamba lengo hilo la Serikali ili liweze kufanikiwa itaendelea kuwekeza katika ujenzi wa miradi mipya na ukarabati wa miradi ya zamani kwa kushirikiana na wananchi katika kuibua, kupanga, kutekeleza pamoja na usimamizi na uendeshaji wa miradi hiyo pindi inapokamilika.

Awali wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Ikungi Mhe. Rahabu alibainisha kwamba  Mwenge wa Uhuru 2021 Wilayani Manyoni utakagua na kuzindua  miradi Mitatu (3) na Programu sita (6)  kama ifuatavyo.

Mapambano dhidi ya Malaria, Klabu ya wapinga Rushwa, Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Ujenzi Wa Mradi wa maji katika kijiji cha Kashangu kilichopo katika Wilaya ya Manyoni na Mradi wa Lishe.   

Pia walizindua programua ya matumizi sahihi ya TEHAMA, Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja, Ujenzi wa Zahanati ya Masigati pamoja na  Ushonaji ambapo yote ilizinduliwa.

Kwa upande mwingine LT. Josephine Paulo Mwambashi kiongozi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru  2021 wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manyoni wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa Mradi wa maji wa kijiji cha Kashangu kilichopo katika Wilaya ya Manyoni amewataka kutunza miradi hiyo ili iwaletee mafanikio wananchi.

Hata hivyo ameipongea wakala wa maji na usafi wa mazingira vijiji RUWASA kwa kazi kubwa walioifanya ya kujenga na kusimamia vizuri miradi ya maji wilayani Manyoni na Singida kwa ujumla na kuwataka kujenga mazoea ya kuweka kumbukumbu vizuri wakati wa utekelezaji wa kazi zao.

Mungu Bariki Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 na Wakimbiza Mwenge Kitaifa

Mungu Ubariki Mkoa wa Singida,

Mungu Ibariki Tanzania

MWENGE WA UHURU HOYEEEEEE!!!!!!!!!

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.