Kijiji cha Mbelekyesye kilichopo Wilayani Iramba Mkoani Singida kimeendelea kunufaika na mawasiliano ya uhakika yenye tija katika nyanja za kiuchumi kutokana na uwepo wa mnara wa mawasiliano kijijini hapo
. Hayo yameshuhudiwa leo baada ya Kamati ya Bunge kufika kukagua ujenzi na utendaji kazi wa mnara huo uliojengwa na mtandao wa Yas kwa ruzuku ya Tshs 124,235,000 kwa usimamizi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Umma UCSAF.
Akizungumza katika hafla hiyo,Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt.Fatuma Mganga amesema uwepo wa mnara huo utarahisisha mawasiliano baina ya watu,lakini pia huduma za kifedha zitakua rahisi sana kwani wananchi watakua huru kufanya miamala ya kifedha katika benki tofauti bila kutembea umbali mrefu kufika kwa mawakala au katika mashine za ATM.
Kadhalika,ameomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kwa kuhakikisha mnara huo unatunzwa vizuri katika kuhakikisha unadumu ili kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Naye Mbunge wa Busega,Simiyu ametoa pongezi kwa wananchi wa Mbelekyese kwa utayari wao wa kutoa eneo la kuujenga mnara huo ambao utakwenda kuwa nguzo kuu katika nyanja ya mawasiliano.Pia ameshauri uwepo wa mitandao mingine katika mnara huo mmoja kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wananchi ambao wanatumia mtandao zaidi ya mmoja
Hamady Nkungu,mkazi wa Kijiji cha Mbelekesye wilayani Iramba ameonyesha kufurahia kuzinduliwa kwa mnara huo ambao amesema unakwenda kuchochea maendeleo ya wananchi kiuchumi ambapo hapo awali yalikua ya taabu na kuzorotesha maendeleo yao ikiwemo kukosa masoko ya bidhaa zao mbalimbali za kilimo na ufugaji.
"Kwa sasa imekua rahisi kupata wateja wa mazao na mifugo yetu kwasababu mawasiliano ya uhakika yanatoweka karibu sana na wanunuzi tofauti na hapo nyuma ambapo tulitumia muda mwingi kutafuta wateja na kutumia muda kidogo katika shughuli za uzalishaji mali"amesema Nkungu.
Kuzinduliwa kwa mnara huu ni utekelezaji wa kujenga minara mingine 758 hapa nchini ambayo itawasaidia wananchi kuingia katika mfumo wa uchumi wa kidigitali.Lengo likiwa ni kupata taarifa muhimu za kukuza uchumi kama vile taarifa za pembejeo za kilimo na mifugo na mengineyo.
Kwa taarifa zaidi(video) tembelea kiungo kifuatacho;
https://youtu.be/nwSJfviccoM?si=P9RmMnwkt73yY4x_
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.