Programu ya Shule Bora imewakutanisha Maafisa elimu Sekondari na Msingi ngazi za Wilaya ili kujadili mipango na mikakati ya Utekelezaji wa programu hiyo baada ya kukamilisha mwaka mmoja.
Akifungua kikao hicho Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Eva Mosha amewataka viongozi hao kuweka mipango inayotekelezwa na yenye mrejesho ili kuisaidia kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa Mkoa huo.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Eva Mosha akifungua kikao hicho.
Aidha amewakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kuhakikisha kwamba mipango hiyo inasaidia kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji pamoja na ujumuishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum na watoto wa kike.
Kwa upande wake Mratibu wa Programu hiyo Samweli Daniel amewaomba waratibu wa elimu ngazi ya Kata pamoja na wakuu wa Shule katika Mpango wa utekelezaji kwa mwaka huu waimarishe usimamizi ili kuleta mabadiliko ya ufaulu.
Mratibu wa Programu ya Shule Bora Mkoani Singida Samweli Daniel, akizungumza wakati wa kikao hicho.
Amesema imebainika kwamba shule nyingi zinashindwa kufanya vizuri kwa kuwa usimamizi unalega lega hivyo ukipata usimamizi madhubuti utaleta matokeo chanya.
"Yupo Mkuu wa Shule kutoka Wilaya ya Mkalama ambaye alihamishwa kutoka shule ikiwemo ambayo ilisifiwa kufanya vizuri na kuonekana shule iliyokuwa inafanya vibaya sana lakini matokeo ya hivi karibuni nayo imekuwa kinara hii inatokana na usimamizi mzuri" alisema Mratibu.
Hata hivyo wajumbe hao wamepanga mambo mengi ya kuimarisha elimu yakiwemo kuimarisha upatikanaji wa chakula mashuleni, kuhakikisha uwepo wa miongozo mbalimbali kwa wakuu wa shule kuendeleza Mafunzo ya walimu kazini pamoja na kuhamasisha wazazi na viongozi mbalimbali kuhakikisha watoto wanaadikishwa katika elimu husika.
Warsha hiyo itafanyika kwa muda wa siku mbili na iliwahusisha Maafisa elimu, Maafisa mipango, Maendeleo ya jamii na walimu wa shule maalum.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.