Wanafunzi wa shule za Sekondari Sekoutoure na Ilongero katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ,katika kijiji cha Sekoutoure, na Tarafa ya Ilongero wameepukana na adha ya msongamano darasani na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi waliokua wakisoma katika shule ya Ilongero Sekondari.
Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa ameweka jiwe la msingi leo tarehe 25 Oktoba 2024 Shule Mpya ya Sekondari Sekoutoure kuashiria uzinduzi rasmi wa shule hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni moja.
Akizungumza maara baada ya kukagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo Waziri Silaa amesema hiyo ni sehemu tu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu nchi nzima ikiwa ni pamoja na Mkoa wa singida.
Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule hiyo mpya iliyoanza rasmi januari 2023 ikiwa na idadi ya wanafunzi 483 hadi sasa kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuwa tayari Serikali imeweka miundombinu bora katika shule hiyo.
Akitoa taarifa ya Mradi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondary Sekoutoure Tatu Njaku amesema ujenzi wa shule hiyo umeboresha mazingira ya Kufundishia na wanafunzi kujifunza.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa ujumla wake amesema kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Singida unashule mpya za sekondari 33 ikiwa ni kuendelea kupunguza changamoto za wanafunzi kusoma umbali mrefu.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.