Muongozo wa uendeshaji wa mashamba ya pamoja ya korosho Wilayani Manyoni Mkoani Singida umetolewa rasmi (block farm) ili kuongeza usimamizi na ubora wa zao hilo na tija iliyokusudiwa.
Muongozo huo umezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemilembe Lwota wakati alipokutana na wadau wa zao la Korosho wa Mkoa wa Singida lengo likiwa ni kuupitisha na kuuzindua kwa ajili ya uendeshaji wa mashamba hayo.
Aidha DC Kemilembe amesema muongozo huo utasaidia kutatua changamoto ya usafishaji wa mashamba, na utoaji wa huduma za ugani kwa kila mkulima atalazimika kufuata utaratibu uliopo kwenye muongozo.
"Leo tutaupitia muongozo wetu wa mashamba ya korosho ambao utasaidia kuhudumia na kusimamia mashamba hayo hasa kusafisha na huduma za ugani" DC Kemilembe.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, Fransis Alfred ameushukuru uongozi wa Wilaya kwa kusimamia kikamilifu uwekezaji wa mashamba ya korosho ambapo amesema kwa mwaka jana wateja wa korosho za Manyoni walisifia kwa ubora na utamu ulizonazo.
Mkurugenzi huyo amesema Bodi imejenga Ofisi na kuweka watumishi Wilayani Manyoni na kuwapatia vitendea kazi kama pikipiki ambazo zitawasaidia kuyafikia mashamba mengi na kutoa huduma za ugani kwa weledi zaidi.
Aidha amewataka wakulima wanaoishi nje ya Wilaya ya Manyoni kuweka vibao vinavyotambulisha majina ya wamiliki pamoja na namba za simu ili maafisa ugani hao waweze kuwasiliana nao kwa ajili ya kuwapa ushauri.
"Tumejenga Ofisi katika mashamba ya pamoja na kuweka watumishi ambao tumewapatia pikipiki ili waweze kutoa huduma kwa wakulima wa Manyoni, Itigi na Ikungi, hata hivyo tunawaomba wakulima wa nje ya hapa kuweka vibao na namba zao za simu ili wataalamu wetu waweze kuwashauri " Fransis
Hata hivyo Mkurugenzi amesema wamejipanga kufanya mnada wa korosho ambapo wakulima wanazo kilo 23,000 sawa na Tani 23 ambapo zitauzwa kwa njia ya mnada.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni, Heri Kaombwe amesema bado Serikali imeendelea kusafisha mashamba hayo na kuyasajili Wizara ya Ardhi ambapo kila mkulima atahitajika kwenda kuchukua ankara zao katika Ofisi hizo.
Hata hivyo amebainisha kwamba baadhi ya changamoto bado zinayakumba mashamba hayo yakihusisha miundombinu mibovu ya barabara ambapo ameeleza kwamba jitihada za kutengeneza zinaendelea.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.