• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

"Hakikisheni chumvi inayotumika inakuwa na Madini joto ya kutosha" Dorothy Mwaluko

Posted on: November 11th, 2022

Maafisa wa Afya na Lishe Mkoani Singida wametakiwa kutembelea mashamba yote ya chumvi yaliyopo Mkoani hapo na kupima chumvi inayovunwa ili kuona kiwango cha Madini joto yaliyomo.

Maagizo hayo yametolewa leo tarehe 11.11.2022 na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mwl. Dorothy Mwaluko alipotembelea mashamba ya chumvi yaliyopo Sekenke kijiji cha Nkonkirangi Wilaya ya Iramba ili kuona kiwango cha Madini joto yanayopatikana katika bidhaa hiyo.

Aidha wataalamu wa afya na Lishe walipima chumvi na kubaini kwamba ina kiwango kidogo cha Madini joto ambapo ndipo Katibu Tawala huyo alipotoa maelekezo kwa wataalamu hao kuyapitia mashamba yote ya chumvi na kupima  viwango vya Madini joto na kuwataka  kuweka mpango wa kuongezea Madini hayo kabla ya kumfikia mlaji.

Mwaluko amewataka wataalamu hao kuanza kutoa elimu kwa wanunuzi wa chumvi hiyo juu ya umuhimu wa madini joto katika mwili wa mwanadamu.

Amesema wanunuzi ndio watakao saidia kuwaelimisha wateja wao kulingana na bidhaa watakayoihitaji.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Lishe wa Mkoa Christowela Barnaba amesema bidhaa hiyo ni muhimu kuongezewa madini joto ili kuepuka kupata ugonjwa wa  goita jambo ambalo linaweza kugharimu maisha ya mlaji.

Amesema pamoja na kukutana na wanunuzi wao wataendelea kutoa elimu kwa wavunaji na wachuuzi pamoja na viwanda kuhakikisha wanauza chumvi ambayo ina kiwango cha kutosha cha Madini joto.

Naye Afisa Afya wa Mkoa wa Singida Mgeta Sebastiani amefafanua kwamba mwananchi anahitaji kuwa na afya bora itakayomsaidia kuzalisha mali na kuongeza kipato na kueleza kwamba ukosefu wa Madini joto inaweza kusababisha kipato kinachopatikana kutumika kujitibia.

Mgeta amewashauri wavuna chumvi hao kutazama Afya zao kabla ya biashara na kuondoa imani potofu kwamba chumvi ikiongezewa madini joto inabadilika rangi na wateja wataikataa.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.