KATIBU Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, ameuagiza Mradi wa Shule Bora unaotekelezwa katika mikoa tisa (9) nchini kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Singida ili kuinua viwango vya elimu mkoani hapa.
Akifungua mkutano wa uhamasishaji wa Programu ya Shule Bora kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya habari leo, amesema walimu watakaopewa mafunzo hayo nao watakwenda kuwafundisha wenzao.
"Kila Halmashauri kuwe na 'trainers' ambapo kutatafutwa 'centre' walimu watakuwa wanakutana na hivyo wataguswa walimu wengi kwa wakati mmoja na mpango huu uanze mara moja mwezi Februari mwaka huu," amesema.
Mradi wa Shule Bora umelenga kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za Serikali zilizopo katika mikoa ya Singida, Dodoma, Simiyu, Tanga, Mara, Rukwa, Katavi, Pwani na mkoa wa Kugoma.
Mkutano ukiendelea
MWISHO
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.