Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amefanya kikao na wajumbe wa vyama vyote vya siasa vilivyopo mkoani Singida Kwa lengo la kusisitiza umoja,amani na utulivu kuelekea siku ya uchaguzi Novemba 27,2024 kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Leo asubuhi kutoka vyama mbali mbali ikiwepo CHADEMA,CUF,DEMOKRASIA MAKINI,UMD,CCM,NLD,NRA,ACT-WAZALENDO,UDP na CHAUMA.
Akizungumza katika kikao hichi amewapongeza wajumbe wa vyama hivyo Kwa kufanya kampeni za amani katika siku zote husika bila uvunjifu wa amani huku akisisitiza kudumishwa Kwa amani iliyopo sasa mpaka tarehe ya uchaguzi itakapowadia na hata baada ya uchaguzi .
"Sisi sote ni ndugu,uchaguzi WA Tanzania ni wa Singida pia,na amani ya Tanzania ni ya Singida pia,sisi sote ni wamoja,tuweke utofauti qa vyama na dini pembeni,Serikali imekamilisha taratibu zote zimeshakamilika,hivyo tarehe 27 ninaomba amani iliyopo muiendeleze na watakaochaguliwa wote tuwaunge mkono."alisema RC Dendego.
Pia amewahakikishia amani na ulinzi na kutosha katika wakati wote wa kampeni na uchaguzi na hata baada ya uchaguzi na kuwakaribisha katika Ofisi muda wowote watakapokua na changamoto akisema kuwa ni vema kutumia upinzani vizuri kwa kujenga maendeleo na amani pamoja na msingi Bora WA uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
"Tunashindana Kwenye sera na mipango,Tutumie upinzani Kwa amani na sera na sio vurugu katika siku ya uchaguzi,Tuijenge amani mwaka huu Kwa msingi Bora WA uchaguzi WA mwaka 2025"alisema RC Dendego.
Naye Mwenyekiti WA Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa wa Singida Hamis Labia, amefurahishwa na kukutana kwa viongozi na wajumbe wa vyama vingine vya upinzani akisema ni njia Bora ya kujenga ukaribu Wenye matokeo chanya ya urafiki na undugu mwema Kwa kuweza kujadili changamoto zao na kuzipatia jawabu Kwa pamoja.
Samweli G.Malo,Katibu WA CHADEMA Mkoa wa Singida amesisitiza uchaguzi WA haki na uwazi Wenye upinzani WA kiitikadi na kisera,akiomba ulinzi kuimarishwa katika kulinda kura zinazopigwa na kusisitiza uaminifu Kwa mawakala.Pia amesema kuwa CHADEMA imetoa wagombea 3,240 katika vijiji 217 kati ya vijiji 442.
Akizungumza katika kikao hicho,Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida amesema kuwa kwasasa mazingira ya uchaguzi yamekuwa ya amani kuliko kipindi Cha nyuma kwani amani imekuwa nguzo muhimu katika wakati wote hasa wakati WA kampeni kwani wagombea wamekuwa wakinadi sera zao Kwa amani na utulivu wa Hali ya juu sana hivyo kufanya zoezi la uchaguzi kuwa la amani na utulivu zaidi katika maeneo yote na wanategemea muitikio mkubwa wa wananchi tarehe ya kupiga kura tarehe 27 Novemba.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.