Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego leo hii ameshuhudia na kukabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa Uongozi wa BAKWATA Mkoani Singida,gafla iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo Februari 15,2025.
Hayo yamejiri baada ya ardhi hiyo iliyopo katika eneo la MANGA iliyodaiwa kupokwa kutoka BAKWATA na mwananchi aliyenunua ardhi hiyo bila utaratibu kinyume na sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego ametoa pongezi kwa uongozi wa BAKWATA na jumuiya ya Waislamu kwa uvumilivu na utulivu wao waliouonyesha wakati wakisubiri suala lao kushughulikiwa.
Pia ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa BAKWATA Mkoani Singida endapo watahitaji kujiendeleza kwa kufanya miradi mbalimbali katika ardhi hiyo sambamba na kuwaasa kutunza vizuri mipaka ya eneo hilo kwa kuweka mipaka ya kudumu kama vile miti ili kuepusha migogoro ya ardhi hapo baadae.
Naye Kamishna wa ardhi msaidizi Mkoani Singida,Bi.Shamimu Hoza amewakumbusha kuzingatia kulipa kodi ya pango la ardhi hiyo kwa wakati na kwa uaminifu ili kuepuka riba ya kuchelewesha kodi hiyo.
Akizungumza baada ya hafla hiyo,Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida,Sheikh Issa Nassoro ametoa shukurani kwa Wizara ya adhi,baraza la ardhi Mkoa wa Singida,kwa kuridhia ombi lao la kurejeshewa ardhi hiyo iliyokuwa imepokwa na kuirejesha katika umiliki wa BAKWATA Mkoani Singida huku akisema kubwa ardhi hiyo itaingizwa katika taratibu za mali za baraza.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.