• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Mahenge akagua uandikishwaji wa wanafunzi wa sekondari na msingi, awataka wakuu wa Shule kushirikiana na viongozi wa Kata kufuatilia ambao hawajaripoti

Posted on: January 18th, 2022

Wakuu wa Shule za msingi na sekondari mkoani Singida wametakiwa kusambaza orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kwenye Shule zao na kuwakabidhi viongozi wa Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji ili viongozi hao wafuatilie nyumba kwa nyumba wanafunzi ambao wamechaguliwa na hawajaripoti  Shuleni.

Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea na kujione hali ya uandikishwaji wa wanafunzi kwa mwaka 2022 katika Shule zilizopo katika Manispaa ya Mkoa wa Singida RC Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema kila mwenye sifa ya kwenda Shule lazima ihakikishwe kwamba anaripoti.

Amesema toka Shule zimefunguliwa tarehe 17 Januari 2022 ni asilimia 54 ya wanafunzi wote ndio ambao wameweza kuripoti katika Shule walizopangiwa hivyo kuwataka viongozi wa kata Tarafa na vijiji kushirikiana na wakuu wa Shule  na kuhakikisha kila aliyechaguliwa anakwenda Shule isipokuwa tu kwa wale ambao wamehamia Shule binafsi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi ambao watoto wao bado hawajaripoti maShule kutumia kipindi cha wiki moja kuhakikisha wanakwenda Shule kwa sababu tayari masomo yameanza kufundishwa.

“Hakuna sababu ya mtoto yeyote kutokuja Shule kwa sababu madarasa yapo ya kutosha, madawati na walimu wapo hivyo  Rais wa Jamhuri ya muungano alileta fedha za kutosha ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi ambeye atashindewa kwenda Shule hivyo kila mzazi ahakikishe kwamba mtoto anasoma.” Alisema Rc Mahenge

Aidha, amewataka wanafunzi wote kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kuweza kufaulu mitihani yao na kufikia ndoto zao ili hiyo iwe kama zawadi ya shukrani kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani ambeye alitoa fedha kwa ajilili ya ujenzi wa madarasa hayo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akamhakikisha Mkuu wa mkoa kwamba katika kipindi cha wiki moja baada ya kufungua Shule watafanya msako kwa kila mtoto ambaye hajafika Shuleni kwa kuwa kila mwanafunzi wa kila kata kwa kuwa kila familia inafahamika.

Amewakumbusha wazazi kuondoa mazoea ya kwamba Shule zikifunguliwa wiki ya kwanza inatumika kufanya usafi na kupanga madarasa, hali ambayo  kwa sasa amesema haipo kwa kuwa kila kitu kiliandaliwa  na masomo tayari yamekwisha anza.

Awali akitoa taarifa ya Manispaa Afisa elimu wa Manispaa hiyo Bwana Jeshi Lupembe amesema jumla ya wanafunzi 3,976 katika Manispaa ya Singida walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza lakini hadi tarehe 17 Januari 2022 ambayo ni siku ya kufungua Shule jumla ya wanafunzi 1,319 ndio walikuwa wameripoti.

Amesema Bw. Jeshi Lupembe kwamba kiwango hicho cha kuwapokea wanafunzi wapya ni dalili kwamba kiwango cha usajili kimeongezeka tofauti na makadirio yao ya awali.

Matukio katika picha

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (kulia) akizungumza katika Shule ya Sekondari Mufumbu iliyopo Kisaki katika Manispaa ya Singida wakati wa ziara hiyo.

Mhe. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Bi. Yagi Kiaratu akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani) wa shule ya Sekondari Mufumbu iliyopo Singida wakati wa ziara hiyo.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.