Wananchi mkoani Singida wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upandaji miti litakalofanyika kimkoa katika maeneo mbalimbali mkoani humo siku ya Jumamosi Januari 29, 2022 ili kuhifadhi na kuyalinda mazingira.
Wito huo umetolewa leo Januari 25, 2022 na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge wakati akikagua hali ya mazingira katika maeneo ya kuhifadhia taka ngumu yaliyopo Msufini, Nyuma ya Uwanja wa Liti, Standi ya Zamani, Stand Kuu ya Mabasi Misuna na Soko Kuu katika Manispaa ya Singida Mjini.
Akiongea na Wananchi hao Mkuu wa mkoa akawataka wananchi hao kujitokeza katika maeneo yao kupanda miti huku wengine wakiendelea na zoezi hilo katika maeneo ya kando ya Maziwa ya Singidani na Ziwa Kindai pamoja na kingo za Mito.
“Leo tumefanya ukaguzi wa usafi wa mazingira katika maeneo yetu ya Manispaa ya Singida lakini kubwa kuliko nitoe wito kwa Wananchi wote wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi Siku ya Jumamosi ya tarehe 29/1/2022 kufanya usafi katika maeneo yetu yanayotuzunguka pamoja na kushiriki katika zoezi la upandaji miti katika kipindi hiki cha mvua” Alisema Dkt. Mahenge
Awali Magreth Mushi Mfanyabiashara wa Soko Kuu aliiomba Serikali kuwatenganishia eneo la kuhifadhia taka ngumu kati yao na wananchi wengine wanaoyazunguka maeneo hayo ili kuleta uwajibikaji, usimamizi na ufuatiliaji katika eneo hilo.
Amesema madampo hayo yasipofanyiwa usafi yanachafua hali ya hewa na nihatari kwa afya za wafanyabiashara na wateja wanoukuja kununua bidhaa zao.
Naye, Zaituni Ismail mmoja wa wafanyabiashara wa maeneo hayo akaiomba Serikali kuhakikisha taka hizo zinazolewa kila baada ya wiki moja ambapo alibainisha kwamba uwepo wa taka hizo kwa muda mrefu zinasababisha kukosekana kwa wateja hasa wa matunda na mbogamboga.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika eneo la Dampo lililoko Soko Kuu kwaajili ya kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati wa ziara yake fupi ya kukagua usafi wa mazingira katika Manispaa ya Singida Mjini
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.