• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Mahenge Azitaka Kamati za Ujenzi wa Madarasa Kuimarisha Usimamizi

Posted on: November 23rd, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo amefanya ziara ya kushtukiza katika shule sita (6) za Sekondari  katika  Manispaa ya Singida Mjini zinazoendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia fedha za UVIKO 19 lengo likiwa ni kujionea hatua iliyofikiwa katika  ujenzi huo na kusisitizia ukamilishwaji ndani ya wakati.

Akiwa katika ziara hiyo Dkt. Binilith Mahege  akazitaka kamati za ujenzi wa shule kutumia muda wao mwingi katika usimamizi wa ujenzi huo ili kupata majengo yenye ubora unaokubalika na kukamilika kwa muda maalum.

Aidha Dkt. Mahenge akakemea vikali kitendo cha kamati za ujenzi wa shule kuwaachia kazi ya usimamizi wakuu wa shule ambapo inafahamika wazi kwamba wanamajukumu mengine ya kusimamia nidhamu na masomo kwa ujumla katika shule zao.

Hata hivyo RC akawataka walimu wakuu wanaosimamia ujenzi huo kuhakikisha kila jengo linakamilika katika kipindi kilichopangwa ambacho ni tarehe  1/12/2021, kwa kuwa kila shule imeonekana kuwa na vitendea kazi vya kutosha.

Dkt. Mahenge akatoa maelekezo kwa watendaji wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri kuhakikisha kunakuwepo na wasimamizi kwa kila jengo linalojengwa mkoani hapa.

Aidha RC akamkumbusha Mkurugezi wa Manispaa ya Singida Mjini Zefrin Kimolo Lubuva kuwatumia wakuu wa Idara mbalimbali waweze kusimamia ujenzi na ikiwezekena kila Mkuu wa Idara apewe mradi wake alifafanua.

Amebainisha kwamba changamoto nyingi ambazo zimeonekana katika ujenzi unaoendelea katika Manispaa hiyo ni usimamizi mdogo ambao umeachwa kwa wakuu wa shule peke yao hivyo kila Mkuu wa Idara apatiwe shule ya kusimamia mpaka ujenzi ukamilike alibainisha Dkt. Mahenge

Awali Mkuu wa Mkoa alitoa pongezi kwa wakuu wa shule kwa namna ambavyo waliweza kuendelea kusimamia ujenzi huo na kufikia hatua nzuri. Shule zilizotembelewa ni  Chief Senge, Mandewa, Kindai Sekondari, Mitunduruni, Unyambwa na Mnyamikumbi kati ya hizo ni shule mbili ambazo zilikuwa zipo hatua ya msingi wakati nyinge zikiwa katika hatua ya linter na kuezeka.  

      Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Pasikas Muragili akafafanua kwamba tayari wameshaunda timu  maalumu ya ufuatiliaji ambayo tayari imeshaanza kazi ili kusaidia usimamizi wa kazi hiyo.

DC huyo amewakumbusha mafundi na wasimamizi wa majengo hayo kwamba siku saba zilizobaki zikitumiwa vizuri uwezekano wa kumaliza kazi hizo ni mkubwa endapo kila saa litatumika vizuri.

Amewataka wahandisi kuendelea kusimamia kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kuhakikisha kunakuwepo na mawasiliano ya kila siku kati yao na Mkurugezi wa Halmashauri ili kuweza kutataua changamoto yeyote itakayoweza kujitokeza.

Naya Mkuu wa Shule ya Sekondari Unyambwa  Bwana Charles Mtaturu amesema moja ya changamoto ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikitatiza ujenzi huo ni upatikaji wa vifaa vya kazi na mafundi kwa ajili ya ujenzi

Bwana Mtaturu amebainisha kwamba viwanda vingi vilikuwa vimeshachukua Maagizo kwa watu mbalimbali na mafundi wengi wamewahiwa katika kazi nyingine kwa kwawa mainisapaa hiyo shule ujenzi wa mashule unafanyika kila mahali.

Yagi Maulidi Kiaratu ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida mjini  akitoa shukrani kwa washiriki wa ziara hiyo amesema ujio wa Mkuu wa Mkoa wa kushtukiza  kutaongeza  chahu na  uhamasishaji   katika kukamilisha kazi hiyo.

Amesema kwa upande wake atashirikiana na  madiwani pamoja na chama Tawala CCM ambapo wataaza rasmi ziara kama hiyo kuanzia kesho tarehe 24/11/2021 kutembelea miradi yote ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Aidha amemalizia kwa kusema  siku zilizobaki zinaweza kukamilisha shughuli zote za ujenzi endapo kila mdau atafanya kazi yake kwa kuzingatia muda na mikakati iliyowekwa.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.