Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba,amekabidhiwa madarasa mpya 29 na Ofisi 11 za Walimu zilizojengwa katika Wilayaya Ikungi na kusema kuanzia mwakani mkoa utaweka mkakati wa kuondoa matokeo yamtihani daraja la sifuri na nne kwa wanafunzi.
Akizungumza baada ya kukagua madarasa yaliyojengwa katika Shule zaSekondari Wilayani Ikungi, Mungaa na Issuna na kuzungumza na wananchi, RCSerukamba alisema Wilaya ya Ikungi imekuwa ya kwanza kati ya wilaya sita zamkoa huo kwa kutekeleza kwa wakati ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Serukamba alisema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenziwa vyumba vya madarasa vitakayowawezesha wanafunzi kusoma katika mazingiramazuri hivyo halitakuwa jambo jema kwa wanafunzi kupata daraja la sifurikutokana na miundombinu bora na mazingira rafiki yanayowezesha upatikanaji waelimu bora kwa mwanafunzi na mwalimu kufundisha.
Alisema Mkoa wa Singida ulipewa na Serikali Kuu Sh. Bilioni 5.8kwa ajili ya kujenga madarasa mapya 290 lakini Mkoa uliamua kuweka mikakatiyake ambapo katika fedha hizo hizo mbali na kujenga madarasa hayo kiasi chafedha kingine kilitumika kujenga shule mpya saba za Sekondari kwa kushirikianana wananchi.
“Kuanzia mwakani nitakutana na walimu shule zote za Mkoa waSingida ili tujadialiane na kupanga mikakati ya namna ya kuondoa matokeo yamtihani ya ‘division zero na four’ kwa shule zote, “alisema RC Serukamba.
Serukamba alisema ili kuondokana na matokeo mabaya, walimuwatimize wajibu wao vizuri wa kufundisha na wanafunzi nao wasome kwabidii kwani baada ya ujenzi wa madarasa haya hakutakuwa na kisingizo tena.
Alisema kati ya Wilaya zote za Mkoa wa Singida, Wilaya ya Ikungikatika ujenzi wa madarasa hayo iliweza ilijiongeza kwa kujenga ofisi 11 zawalimu ambazo hazikuwepo katika bajeti ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Naye Mkuu wa Wiaya ya Ikungi, Jerry Muro, alisema ushirikiano waviongozi na wananchi katika Wilaya hiyo ndio umesaidia kufanikisha kukamilikakwa wakati ujenzi wa madarasa hayo.
Muro aliishukuru Serikali kwa kutoa kiasi cha Sh. Milioni 580 kwaajili ya ujenzi wa madarasa hayo na kwamba Serikali Wilayani humo itaendeleakusimamia na kutekeleza miradi yote ambayo Serikali imetoa fedha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Justice Kijazi alisema mwezi Septemba mwaka huu Halmashauri hiyo ilipokea kiasicha Sh. Milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 29 katika shule16 za Sekondari.
Alisema baada ya kupokea fedha ziliingizwa kwenye akaunti ya shulehusika na ujenzi ukaanza ambapo mbali na kujenga idadi hiyo ya madarasalakini pia madawati 1160, meza 1160 na viti 1160 yametengenezwa kwa ajili yamapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.
Mbunge wa Ikungi Mashariki Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Ikungi waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.