Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida umejipanga kukagua miradi yenye thamani ya Bilioni 8.28 ikiwa ni jumla ya miradi 35 inayohusu Elimu, Afya, Utawala bora, Maji, Barabara na uwezeshaji wa vijana kiuchumi.
Akihutubia leo tarehe 09.08.2022 Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mseko kilichopo Wilaya ya Iramba amesema kiasi hicho cha fedha kimejumisha Tsh.Milioni 84.203 ikiwa ni michango ya wananchi, Tsh.Milioni 173.29 ikiwa ni kutoka Halmashauri, Bilioni 6.449 kutoka Serikali Kuu na fedha kutoka kwa wahisani Sh.Bikioni 1.575.
Aidha amebainisha kwamba programu 18 zitazinduliwa na 11 zitawekewa jiwe la msingi ikiwa ni pamoja na programu 42 za Sensa, Rushwa, Malaria, Mapambano dhidi ya dawa za kulevya VVU na miradi ya Lishe.
RC Serukamba akaeleza kwamba katika kipindi cha awamu ya Sita Mkoa wa Singida umepokea jumla ya Tsh.Bilioni 270.371 kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na kwa wadau wengine kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya Utawala bora Kilimo Uwezeshaji wa vijana Sekta ya Barabara Nishati Maji na Habari na Mawasimiano.
Amesema sekta ya Afya jumla ya Sh.Bilioni 28.4 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali Nne (4), vituo vya Afya 15 na Ujenzi wa Zahanati utoaji wa chanjo na Ujenzi wa vyoo katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Aidha RC Serukamba amesema miradi mingine ni ya sekta ya Kilimo ambapo wakulima walipatiwa mbegu za ruzuku ya Serikali yenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.26 zilizotolewa kwa wakulima wa Mkoa huo.
Hata hivyo amesema jumla ya vikundi 409 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vimefaidika na mfuko wa Taifa wa TASAF na kugharimu Tsh. Bilioni 12.07
Kwa upande wake Sahili Nyanzabara Geraruma Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amezitaka kila Halmashauri kuhakikisha wanakuwa na nyaraka halisi zinazohusiana na miradi mbalimbali wakati wa ukaguzi.
Amesema kila Halmashauri inatakiwa kuonesha vielelezo vya namna ilivyo peleka fedha kwa vijana ikiwa ni pamoja na miradi iliyoanzishwa.
Amesema ni muhimu kuongeza usimamizi wa miradi ili iweze kuwasaidia wananchi kwa muda mrefu.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.