Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manyoni kuhakikisha anamaliza mgogoro uliopo wa mashamba ya korosho ambayo wakulima waliuziwa lakini bado hawajaoneshwa mashamba yao na wengine wakiwa bado hawajasafishiwa wakati walikwisha lipia fedha hizo.
Kauli hiyo ameitoa tarehe 09/09/2022 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo alipokutana na Madiwani pamoja na watendaji wa kata na vijiji ambapo amesema katika kipindi chake cha uongozi wa Mkoa huo asingependa kusikia migogoro ya ardhi hasa katika Kilimo.
RC Serukamba ameagiza kuitishwa kikao cha wenye mashamba ambao wamelipia na hawajaoneshwa mashamba yao na wale ambao hayajasafishwa huku akimtaka Mkurugenzi huyo kuhakikisha kila mtu anapata haki yake.
Amesema hakuna mwenye shamba ambaye atapoteza haki zake ilimradi Sheria na taratibu zimefuatwa
Amewataka wakulima wa Wilaya hiyo kuongeza ukubwa wa mashamba ili mazao na kipato kiweze kuongezeka.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.