Walimu na Wazazi Mkoani Singida wameaswa kuyaangalia upya na kuyasimamia maadili na nidhamu kwa wanafunzi ili kupata wazazi na viongozi bora wa baadae kwa manufaa yao na wengine.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba alipokuwa akihutubia umati wa watanzania waliohudhuria Kongamano la kuelekea siku ya kiliele cha Muungano lililofanyika katika ukumbi wa Social Katoliki uliopo mjini Singida.
Serukamba amesema wanafunzi wengi wanaonekana kutokuwa na uvumilivu wa changamoto zozote zinazowakuta katika safari zao za maisha hivyo akaeleza kwamba kwa mtazamo wake ni vigumu kwa mwanafunzi asiyekuwa na uvumilivu kufika mbali ki masomo huku akibainisha kwamba yeyote aliyefanikiwa ki elimu ilitokana na kuwa na uvumilivu.
Aidha amesema maadili ya vijana yamekuwa yakiporomoka siku hadi siku huku akitolea mfano wa baadhi ya wanafunzi wa shule za Sekondari ambao kwa sababu sizizofahamika waliamua kuondoka kwenye mdahalo wakati walimu wao na wageni wengine angali wakiwepo.
"Mtu asiyependa historia ya nchi yake ni mtumwa, tupo hapa kujifunza na kuelewa historia ya Muungano wetu, nilitarajia kwa uwingi wa wanafunzi waliokuwepo toka mwanzo ungeendelea hadi mwisho kwa kuwa ni sehemu ya masomo yao lakini naona idadi yao imeendelea kupungua huu ni ukosefu wa maadili" alisema RC Serukamba.
Amewataka wazazi na walimu kwa pamoja kuendelea kuwafundisha na kuyasimamia maadili ya vijana wote kwa ujumla ili kujenga kizazi chenye maadili ili kupata viongozi na Wazazi bora wa baadae.
Ametoa wito kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwataka kujifunza lugha zaidi ya moja ili iwe rahisi kwao kupambana na soko la ajira badala ya kutumia lugha ya kiswahili pekee kama baadhi yao walivyohoji wakati wa mdahalo kuhusu kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na ujifunzaji.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akihutubia wananchi mbalimbali waliojitokeza katika kongamano la maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika 25/4/2023 ki mkoa katika ukumbi wa mikutano Social Katolika Mjini Singida.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akizungumza na wananchi katika kongamano la maadhimisho ya sherehe za Muungano.
Kongamano la maadhimisho ya Muungano likiendelea
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.