Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa chini ya mradi wa boost ambapo amesema ifikapo tarehe 4 Aprili, 2023 apate taarifa ya utekelezaji ujenzi ulipofikia.
Maelekezo hayo ameyatoa leo tarehe 24.04.2023 wakati alipokutana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote pamoja na maafisa elimu wa Wilaya kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa katika miradi hiyo.
Amesema ifikapo tarehe 30.5.2023 kila Halmashauri iwe imekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa huku akiwakumbusha kuhakikisha wanaanza kutafuta madawati kwa ajili ya vyumba hivyo pamoja na ujenzi wa vyoo.
Aidha, kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amewataka Wakurugenzi hao na wahandisi kuhakikisha katika ujenzi wa vyumba hivyo wakikishe kinapatika ofisi kwa ajili ya walimu ili kuepusha utaratibu wa kutoa chumba cha darasa kutumika kama ofisi.
Hata hivyo amewataka wahandisi wa Mkoa na Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa kikamilifu na kuhakikisha madarasa yanawekwa sakafu za marumaru.
Pamoja na mambo mengine amewataka Makatibu Tawala wasaidizi ambao ni walezi wa Halmashauri kuhakikisha wanasaidia kutoa miongozo ili kufanikisha zoezi hilo kwa wakati.Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (katikati) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatma Mganga (kushoto) pamoja na Afisa Elimu Mkoa Dkt. Elpidius Baganda wakati wa kikao hicho.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi. Aika Mathawe (kulia) akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa chini ya mradi wa boost kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati wa kikao hicho.
Kikao kikiendelea
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.