• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SERUKAMBA AZINDUA UJENZI MRADI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI MSINGI, UTANUFAISHA WANANCHI 12,000

Posted on: June 14th, 2023

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, leo (Juni 14, 2023) amezindua Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji utakaogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 34. 176 utakaotekelezwa katika Kijiji cha Msingi, Kata ya Msingi Wilayani Mkalama mkoani Singida.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18, alisema Mradi wa Skimu ya Msingi utakuwa na jumla ya eneo la hekta 2,000.

Serukamba alisema mradi huu utakapokamilika utawanufaisha wakazi 12,000 kutoka Vijiji vinne vya Ishinsi, Ndurumo, Msingi na Kidi vilivyopo Kata ya Msingi Tarafa ya Kinyangiri ambao watalima mazao ya mpunga, mahindi na mbogamboga kwa misimu miwili hadi mitatu kwa mwaka.

Alisema shughuli kuu zitakazofanyika katika shughuli ya ujenzi wa mradi ni ujenzi wa bwawa lenye ujazo wa Lita 1,875,000, ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji yenye kilometa 19.12, uchimbaji wa mifereji ya matupio yenye urefu wa kilo mita 42.539, uchimbaji wa mifereji ya kuingiza maji mashambani yenye urefu wa jumla ya kilometa 34.778.

Shughuli nyingine zitakazofanyika ni ujenzi wa barabara za mashamba zenye urefu wa kilomita 36.1, kusawazisha ekari 2,000 za mashamba, ujenzi wa kilomita nane za barabara na makaravati sita kuelekea ndani ya mradi na ujenzi wa vigawa maji 14, vipunguza mwendo, viumbo angalizi 90, vipitisha maji 90, makaravati 14 pamoja na vivuko nane.

Mkuu wa Mkoa alisema ili Mkandarasi aweze kuendelea na kazi za ujenzi bila kukwama Tume ya Umwagiliaji ihakikishe inamlipa Mkandarasi kila anapokamilisha hatua mojawapo ya ujenzi.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vitakavyonufaika na mradi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la mradi, Mkuu wa Mkoa huyo aliwataka wananchi kutouza ardhi kwani lengo la Serikali ni kutaka wenyeji wafaidike na mradi huo.

Serukamba aliwaondoa hofu wananchi kwamba watanyang'anywa ardhi kwamba hizo ni propaganda hakuna atakayenyang'anywa na kuagiza wenyeviti wa vijiji kusimamia kuhakikisha kila mwananchi anapata eneo la kulima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymondi Mndolwa, alisema pamoja na kwamba sio jukumu la Tume hiyo kujenga barabara lakini katika mradi huo zimetengwa fedha kwa ajili ya kujenga kilometa nane ili kuwawezesha wananchi kupata urahisi wa kusafirisha mazao yao kutoka mashambani.

Alisema katika mwaka wa fedha ujao Tume hiyo itajenga ghala la kuhifadhia mazao katika kata hiyo ya Msingi ili wakulima wakishavuna wanayahifadhi kwa ajili ya kusubiri kuyauza na kwamba ni jukumu la viongozi wa kijiji kutenga eneo litakapojengwa ghala hilo.

Mndolwa alisema wakati Serikali inajenga miundombinu hiyo ya umwagiliaji wakulima wana wajibu wa kulipa ada ya umwagiliaji fedha ambazo zitakuwa zinawekwa kwenye akaunti maalum ambazo zitatumika kwa ajili ya ukarabati na uendelezaji wa sehemu nyingine zenye miradi hapa nchini.

“Wakati mnaushangilia mradi huu mjue kwamba mtakuwa na miundombinu mizuri mkilima vizuri lakini mtapaswa kulipa ada ya umwagiliaji, msipolipa nitafunga bomba na nitalifunga bomba sio kwa macho hautaniona nitafunga kwa mtandao kwa hiyo huna pa  kunikamatia,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi wa kata hiyo kumsimamia Mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji ili akamilishe mradi huo kwa wakati lakini pia kuhakikisha hawamwibii vifaa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali, alimshukru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha  za ujenzi wa mradi huu na kwani utasaidia kuinua uchumi wa Wilaya hiyo.

Kwaupande wake  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega, alisema fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mradi huu ni nyingi hivyo watahakikisha wanautunza ilu wanufaike na kubadili maisha ya Wananchi.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Pancras Steve akitoa utambulisho wa viongozi mbalimbali walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi, Paskas Muragili akitoa akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Wilaya wa mkoa wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akizungumza na wananchi wa vijiji vitakavyonufaika na mradi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la mradi

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymondi Mndolwa, akizungumza na wananchi wa vijiji vitakavyonufaika na mradi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la mradi.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia makabiadhiano ya mradi huo.

Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya mradi.



Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.